CHONGOLO AAPA CCM KUTORUDI NYUMA SUALA LA BANDARI, AWAALIKA MEZANI WATAALAMU WA SHERIA KUREKEBISHA VIPENGERE VYA MKATABA, WASIRA ALIPUKA NA TAMAA ZA URAISI 2025

Na Joseph Ngilisho Arusha


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema CCM haitarudi nyuma kuhusu uwekezaji wa bandari na amewaalika wataalamu na wajuzi wa sheria kuja mezani ili kurekebisha baadhi ya vipengere vya mkataba ili kulete tija zaidi kwa maendeleo ya nchi.

Alisema mkataba huo ni wa CCM sio wa mtu mmoja na amesisitiza  kuwa suala hilo lipo kwenye ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020,akidai kuwa jambo hilo linaenda kuongeza tija kwa nchi na ccm haipotayari kurudi nyuma.

Chongolo amesema hayo jijini Arusha, wakati akihutubia wananchi wa mikoa ya kanda ya kaskazini ,Arusha,Kilimanjaro  na Manyara katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Chongolo alisema kuna watu wamejipanga kutengeneza uongo ili kusapoti dhamira ya kupotoshaji uboreshaji wa bandari nchini.

"Tunasema haya tukiwa na nguvu tukiwa kifua mbele na hatutarudi nyuma, jambo hili linatija kwa taifa na kwa wananchi,nisisitize kuwa wataalamu na wajuzi wa sheria ambao wanamaoni na ushauri namna ya  kurekebisha baadhi ya vipengere ili kuboresha zaidi ,waje mezani na si vinginevyo "

Naye mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, alisema chanzo cha upotoshaji kuhusu uwekezaji wa bandani ni siasa za uchaguzi wa mwaka 2025, ambapo baadhi ya watu wanamezea mate urais.

Alisema lengo la mkutano huo ni kutoa elimu ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania na Dubai, kuhusu uendeshaji wa bandari ya Dar Es Salaam,

Wasira alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani wengine walidhani atashindwa katika kipindi cha miezi sita, hivyo kutokana na anayoendelea kutekeleza, suala la bandari linapotoshwa na baadhi ya watu wanaoimezea mate nafasi hiyo.

"Kwenye bandari tunahitaji ufanisi kutoka duniani, hao waliowekeza kwenye madini walipatikanaje, kwani walipigiwa kura, waliojenga hoteli Serengeti mliwapigia kura? Amehoji kada huyo wa CC

"Ubaya ni siasa, tena siasa za uchaguzi za mwaka 2025; watu wanaumezea mate urais. Rais Samia alipoingia, waliona yeye ni wa muda, atashindwa baada ya miezi sita; wanafanana na hadithi ya fisi na mkono wa mtu hilo ndiyo tatizo letu."

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakidete alisema sababu kubwa ya kutafuta mwekezaji kwa bandari hiyo baada ya kuona meli nyingi za mizigo zinasimama muda mrefu kusubiri kushusha shehena kwa sababu ya ukosefu wa zana kutosha.

Mwakidete alifafanua sababu za kupangisha bandari ya dar es Salaam ni pamoja na kuwa na Teknolojia  duni ambayo haiendani na kasi na uwezo wa meli tulizonazo na kwa siku moja meli moja inaweza kusubiri zaidi ya siku tano na kwa siku moja gharama ya kusubiri ni dola za kimarekani  elfu 25 sawa na sh, milioni 58 za kitanzania.

"Kwa siku moja gharama ya kusubiri kushusha mzigo ni dola 25,000 sawa na Sh mil.58 na zikiwa siku 10 ni milioni 580,000 na hizo gharama zinabebwa na aliyekodi meli na huyo mwenye mzigo inapelekea kupandisha bei ya bidhaa zake na ndio maana unasikia Bidhaa zinapanda bei"
Mwakidete alitaja udhaifu mwingine wa mamlaka ya bandari  ya dar es salaam ni suala la kimifumo ya Tehama  kutosomana na taasisi mbalimbali kunakosababisha upotevu wa mapato .

Alitolea mfano mwaka 2021 fedha iliyokusanywa na mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, katika bandari ya dar es Salaam ni sh, bilioni 795.2 huku gharama za uendeshaji ikifikia sh, bilioni 791.8 na kiasi kidogo cha sh, bilioni 3.3 kikibakia kama Faida.

Vile vile, sababu nyingine ni za ushindani, baada ya nchi za Uganda, Jamuhuri ya Congo, Rwanda, Zambia na Malawi, kupunguza kushusha mizigo yao kwenye bandari hiyo, huku sababu ikitajwa ucheleweshaji wa mizigo na hivyo kupitisha mizigo yao nchi shindani.

Alisema mapato yanayokusanywa  na TRA kwa sasa ni sh, trillion 7.76 ila kwa mwekezaji akipatikana Mapato yatapanda na kufikia sh trillion 26 fedha ambazo zitasaidia katika sekta mbalimbali za maendeleo nchini.

"Uwekezaji huu sio mgeni tulikuwa ba mwekezaji wa bandari  wa kampuni ya Ticts ambaye alifanyakazi kwa miaka 22 lakini baada ya kuona tija yake ni ndogo tumeamua kumleta mwekezani mwingine ambaye ataboresha bandari na kuongeza Mapato zaidi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Uwekezaji na Mitaji Jerry Slaa, alisema mpaka sasa hakuna mradi wowote unaoendelea kuhusu uwekezaji wa bandari hadi mikataba mingine miwili itakaposainiwa.

Alisema uwekezaji huo utafanyika hatua kwa hatua kwa kuzingatia sheria za nchi na maslahi mapana ya Taifa na hautajumuisha uwekezaji katika bandari ya Tanga na Mtwara pamoja na sekta ya ardhi.

Ends..
Wasemavyo makada wa ccm ,kuhusu Bandari.
Salome Mnyawi, diwani Mererani 

"Suala la bandari tumelipokea kwa mikono yote ni jambo la maendeleo na sio suala la kudidimiza watanzania kama ambavyo zinaenezwa kwa sasa, kuwa bandari imeuzwa michakato ndo imeanza,tuiamini serikali ,kama tumeshindwa kuibiwa tukiwa watoto, tutaibiwa tukiwa wazee"

Edward Ole Lekaita, Mbunge Kiteto

"Kupitia mkutano huu wananchi wamepata elimu,na elimu hii kubwa wataitumia kuwaelimusha wengine na kuondoa Janga la upotoshaji, propaganda hizi zinaenezwa na wale tulioshindana nao kwenye uchaguzi ulioisha tukawashinda"
 
Simoni Maxmilian ,Mwkiti UVCCM Mkoa wa Arusha 

"Ujio wa DP World katika bandari yetu kutaongeza ajira na fursa kwa vijana, na pato la bandari  litapanda kutoka trillion 7 ya sasa hadi kufikia trillion 26 vijana niwaombe na niwasihi tumuunge mkono rais Samia Suluhu hawezi kutupotosha "

Post a Comment

0 Comments