1000 KUTIMUA MBIO ARUSHA MOYO MARATHON, KUCHANGIA TIBA MARADHI YA MOYO KWA WATOTO,WASHIRIKI KUPIMA AFYA BURE HOSPITALI YA MOYO MEDICARE CLINIC


 Na Joseph Ngilisho, Arusha


Washiriki 1000 wanatarajiwa kushiriki mashindano ya riadha ya  Arusha Moyo Marathon,' yaliyopangwa kufanyika jijini Arusha Julai 30 mwaka huu. 


Mbio hizo za Arusha moyo marathoni zitafanyika kwa mara ya kwanza  zikiandaliwa na hospitali ya Moyo Medicare clinic yenye makao yake jijini Arusha zikilenga kusaidia watoto wenye matatizo ya moyo.


 Katibu wa mbio hizo Arusha Moyo Marathon, Hosiana Michael, alisema Mbio zitahusisha,  kilomita 21, kilometa 10, na kilomita 5 
 na zitaanzia na kumalizika  katika  viwanja vya AICC Soweto vilivyoko  Kaloleni jijini hapa.

Alisema mbio hizo zitalenga zaidi changizo la kupata kiasi cha sh,milioni 100 ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye maradhi ya Moyo ili kuokoa maisha yao.

Katibu wa chama cha riadha mkoa Arusha(ARAA) Rogath Steven mbio hizo zimekuwa zikisaidia Kuibua na kuwaandaa wanariadha wanaochipukia na kusema dhumuni lililopo litawapa Faraja watoto wenye matatizo ya moyo.
Naye mganga mfawidhi katika hospitali ya Moyo Medicare,Dk. Iddy Yanga alisema kituo hicho kilianzishwa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za kibingwa na  wamejikita zaidi katika magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo sukari, shinikizo la damu na magonjwa mbalimbali ya moyo.

Alisema wamelenga kuchangisha fedha na zitakazopatikana katika mbio hizo zitatumika kwenda kugharamikia matibabu ya watoto hao ambayo wanaozaliwa na shida ya moyo na tunatarajia kugharamikia watoto 30 katika matibabu .

Naye Mkurugenzi wa hospitali hiyo dkt Felex Masenge alisema kuwa washiriki wa mbio  hizo watapata fursa ya kupima bure magonjwa ya moyo na watakaobainika kuwa na maradhi hayo ama viashiria  wataelekezwa namna ya kupata matibabu.

Ends...












.

Post a Comment

0 Comments