Na Joseph Ngilisho Arusha
Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania wameiomba serikali kusitisha zoezi la kubadili vijiji 14 na kuwa pori tengefu la Pallolet ili kulinda, kuhifadhi na kuendeleza haki za binadamu kwa wananchi wa Tarafa ya Loliondo na sehemu ya Tarafa ya Sale katika wilaya ta Ngorongoro Mkoani Arusha.
Ombi hilo limekuja baada ya watetezi hao kufanya ziara mwezi Mei katika vijiji vya Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga, Tarafa ya Loliondo na Sale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha ili kuangalia hali ya haki za binadamu na kubaini hali mbaya kwa wananchi hao na mifugo yao.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la elimu ya uraia na msaada wa kisheria (CILAO) ODERO ODERO aliwaambia waandishi wa habari jijini Arusha kuwa watetezi wa haki za binadamu wamegundua ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za ardhi, vijiji na uhifadhi wa wanyamapori
Alisema ukiukwaji mwingine ni Watu kupigwa na kuumizwa wakati wa utekelezaji wa zoezi la kutwaliwa ardhi za vijiji hivyo, Viongozi na wawakilishi wa wananchi kukamatwa na kubambikiwa kesi ya mauaji na kisha kufutiwa kesi baada ya kukaa mahabusu kwa takriban miezi 6 na kuachiwa baada ya Jamhuri kusema haina nia ya kuendelea na kesi hiyo
‘'Wananchi 92 walikamatwa na kufunguliwa shitaka la kuingia na kukaa nchini kinyume cha sheria kwa madai kwamba sio raia na baadaye kuachiwa huru na mahakama baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha madai yao au kudai haina nia ya kuendelea na kesi yao.” Alisema Odero.
Alisema wameshuhudia Ukamataji na utaifishaji wa mifugo na kupiga faini kubwa kwa kile kinachodaiwa kwamba mifugo hiyo imeingia kwenye eneo la pori la Pololeti na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwasababishia umaskini mkubwa wananchi hao.
Alisema Mifugo imekufa kwa sababu ya kukosa eneo la malisho, maji na chumvi na kusababisha Umasikini kwa wananchi kutokana na kupoteza mifugo, utaifishaji,mifugo kufa kutokana kukosa maji na majani kwani eneo lililochukuliwa ndilo llikuwa tegemeo la wananchi kufanyia shughuli za ufugaji.
Ends...
0 Comments