Na Joseph Ngilisho, SIMANJIRO
Watu wawili wakazi wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara wanaotuhumiwa kuvunja na kuiba sh,milioni 47 za mfanyabiashara, wanatarajia kufikishwa mahakamani kesho Jumatatu Juni 12,
Kamanda wa polisi mkoa wa Mamishna wa polisi (ACP) George Katabazi akizungumza Juni 11, 2023 amesema watuhumiwa hao Juma Athumani (23) na Mariam Mbega (26) wanatarajiwa kufikishwa mahakama ya wilaya ya Simanjiro.
Kamanda Katabazi amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kuvunja nyumba na kuiba Sh,milioni 47 za mfanyabiasharaLawrent Elias mkazi wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro,
“Polisi waliwafuatilia watuhumiwa hao hadi Handeni mkoani Tanga na jijini Dar es salaam na kuwakamata hivi sasa wapo kituo cha polisi Mirerani na jumatatu ijayo kesho Juni 12 tutawafikisha mahakani Simanjiro,” amesema.
Hata hivyo, mfanyabiashara anayedaiwa kuibiwa fedha hizo, Elias ambaye kitaaluma ni mlipuaji miamba ya Tanzanite, amewapongeza polisi kwa kufanikisha kuwakamata watuhumiwa hao kwani wameonyesha juhudi kubwa na uadilifu wa hali ya juu.
“Namshukuru mkuu wa polisi (IGP) Camilius Wambura, kamanda wa polisi Manyara Katabazi, mkuu wa kituo cha polisi Mirerani Dominick Fwaja, kwa kufanikisha hili,” amesema Elias.
Amesema polisi wanastahili pongezi nyingi kwani, baada ya uhalifu huo watuhumiwa walizificha fedha hizo benki kwenye akaunti zao ili wasibainike na kukamatwa.
Amedai kuwa mbali na fedha pia watuhumiwa hao waliiba simu mbili ndogo na kurunzi (tochi) ambazo pia polisi waliwakamata na vielelezo hivyo vipo polisi.
0 Comments