Na Joseph Ngilisho ,Arusha
WAKATI Bunge la bajeti la Jumuiya ya Afrika Mashariki EALA, likiendelea kwa kishindo katika makao makuu ya jumuiya hiyo ,kamati ya sheria ,haki na Ardhi imeshauri baadhi ya sheria kufanyiwa marekebisho ili kuwezesha baadhi ya mikataba kufanyiwa marekebisho pamoja na lugha zinazopaswa kutumika.
Akiwasilisha taarifa ya kamati katika bunge hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Haki na Ardhi, Mashaka Ngole alitoa rai kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Peter Mathuki kuangalia sheria zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho ili kuwezesha baadhi ya mikataba kurekebishwa sanjari na lugha hizo na kingereza kuweza kutumika.
Kwa mujibu wa Ngole kamati hivyo imefanya ziara kwenye taasisi za EAC katika nchi mbalimbali na kubaini kuwa zinashindwa kutekelezwa majukumu yake kutokana na sheria na baadhi ya vipengele kwenye mkataba wa uanziahwaji wa nchi za EAC kutofanyiwa marekebisho licha ya wakuu wa nchi wanachama kuelekeza marebisho Hayo kufanyika.
“Wajumbe wa kamati hii wametembelea taasisi zote zinasimamiwa na EAC katika nchi mbalimbali wanachama na kuona changamoto zinazowakabili watumishi wa taasisi hizo. Hivyo tunatoa rai kwa nchi hazijatoa ardhi zilizoahidi kwa akili ya ujenzi wa ofisi za Taasisi hivyo watoe ili ujenzi uweze kuanza wa majengo ya kudumu”
Naye Mbunge wa EALA kutoka nchini DR Congo, Masirika Dorothee alisema mabadaliko ya sheria mbalimbali katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni muhimu katika kuwezesha baadhi ya wabunge wa bunge hilo kununua vifaa ili kuwezesha wabunge wasiojua Kiswahili wala Kifaransa kutambua kinachoendelea ndani ya bunge.
Alisema ni lazima mikataba hiyo itambulike na kuwezesha lugha hizo ikiwemo Kingereza kutumika ili kuwezesha wabunge wengi kuchangia mada mbalimbali ili wananchi waweze kuelewa kinachoendelea.
Alisema sheria zisizotekelezeka zilizotungwa na Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) zinakwamisha baadhi ya mambo mbalimbali kutotekelezeka kwa wakati.
Aidha ununuzi wa vifaa vya kutafsiri lugha ni muhimu kwa baadhi ya wabunge lakini bado ni changamoto ya kuvinunua sababu ya baadhi ya sheria hazijarekebishwa za kuwezesha lugha ya Kifaransa na Kiswahili kutumika kama lugha rasmi ndani EAC.
Ends....
0 Comments