Na Joseph Ngilisho, Arusha
Viongozi wa Dini jijini Arusha wameitaka serikali kutoa msimamo kuhusu sakata la mapenzi ya jinsia moja hapa nchini na kupeleka muswada wa sheria bungeni ili kutungwa sheria kali itakayo wabana watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga.
Wakiongea katika maandamano ya kupinga ushoga,ukatili na matukio ya unyanyasaji yaliyoandaliwa na kamati ya Amani ,haki na upendo yaliyofanyika katika uwanja wa sheikh amri abedi jijini Arusha.
Viongozi hao walimtuma mkuu wa mkoa jiji la Arusha,John Mongella kupeleka ujumbe mahususi kwa Rais Samia suluhu Hasan wakimwomba atoe tamko juu ya msimamo wa serikali kuhusu
Sakata la ushoga hapa nchini,kama ambavyo rais wa Uganda Yoweli Museveni ali vyolivalia njuga na kupitisha sheria kali ya ushoga nchini humo.
Mchungaji dkt.Yoseph Otieno wa kanisa la Wadventist alisema halitoshi jambo hilo kupingwa kwa maandamano pekee, bali inapaswa kutungwa sheria kali itakayowabana wanaojihusisha na mchezo mchafu wa mapenzi ya jinsia moja hali inayoweza kuepusha taifa kukosa nguvu kazi ya vijana .
"Maandamano peke yake hayawezi kutatua matatizo kinachoweza kutatua matatizo ni kama Kilichofanyika Uganda ni taifa kuamua kwa dhati na kupeleka msuada kwenye bunge na kutunga sheria ili watu wanaofanya haya wakabiliwe na mkono wa dola"alisema
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT )Dayosisi ya Kaskazini Kati, Solomon Masangwa alimwomba Rais Samia Suluhu Hassan kufanya kama alicho fanya Rais wa Uganda , Yoweri Museven juu ya kuweka sheria kali ya kupinga ushoga.
"Tusiukaribishe utamaduni huo wa kigeni maana tutakuja kuishia mahali pabaya maana hakuna ongezeko la mwanandamu linalo tokana na mapenzi ya jinsia moja niwazi kwamba mpango huo wa ushoga ni kufuta mpango wa mwanadamu kuzaliana kama lilivyo agiza neno la mungu " Enendeni Mkaujaze ulimwengu". Alisema Askofu Masangwa.
Naye kiongozi wa dini ya Sunni,Suleiman Ayubu alisema anakubaliana na maamuzi ya viongozi wenzake wa dini kuwa suala hilo linapaswa kutungiwa sheria kali itakayowabana watu wanaojihusisha na mchezo mchafu wa ushoga na kuwaomba viongozi wenzake kuendelea kupiga vita hiyo ili kutokomeza ukatili,ushoga na unyanyasaji.
Naye katibu wa kamati ya maridhiano ,Mch. Israel Maasa alitoa rai kwa kiongozi mkuu wa serikali, Rais Samia kutoa msimamo wa nchi ili taifa lijue mwelekeo kuhusu ushoga hapa nchini.
"Wito wetu tunaomba bunge litoe tamko juu ya utungwaji wa sheria ya kupinga ushoga hapa nchini ,leo tumefanya maandamano lakini haitoshi kumaliza tatizo hili"
Kwa upande wake kiongozi wa mila wa kabila la Wameru (Mshili), Esrom Sumari alieleza namna walivyofanikiwa kudhibiti matukio hayo kwa kusimamia adhabu ya fimbo 70 kwa vijana wanaoenda kinyume na matakwa ya mila zao na wamekomesha matukio ya ulevi, ukatili,unyanyasaji na ushoga.
Laigwanani Elikisongo Meijo Kiongozi wa kabila la maasai nchini Tanzania, aliwatupia lawama wazazi kwa kushindwa kusimamia malezi bora kwa watoto wao hali inayopelekea kuwepo kwa wimbi la ushoga na kuwaomba wazazi watilie mkazo suala la watoto wao kufanyakazi na kujiepusha na utandawazi usio na tija.
Awali Kamanda wa Polisi wilaya ya Arusha ( OCD ) ASP George Malema alitoa takwimu, akidai kwamba kila siku makosa ya ulawiti hayapungui matatu na wahanga wakubwa wa matukio hayo ni watoto wa shule za msingi.
"Kwa takwimu za nchi Arusha ni Mkoa wa tatu kwa matukio ya ukatili wa kijinsia na ulawiti wa watoto wadogo, na haya yote yanaanzia shuleni, niwaombe viongozi wenye dhamana kuzichukulia hatua kali shule hizi maana mpaka sasa zipo shule zenye alama ya upinde ambao unahamasisha ushoga hayo yote ni kutokana na misaada mbali mbali wanayo ipata pasipo kujali watoto wetu wanaathirika". Alisema OCD Malema.
Akipokea maombi hayo ya viongozi wa dini pamoja na viongozi wa mila Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela alieleza kwamba atafikisha maombi hayo kwa Rais Samia.
Mongela alieleza kwamba Kunahatari kubwa sana kwa vijana baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba baadhi ya shule zinafundisha watoto maswala ya ushoga.
"Kwangu mimi naamini huu ni mpango maalum uliopangwa na wengine huko duniani, Ujumbe huu mimi nitaufikisha kwa Rais Samia Samia ili yeye kama kiongozi wetu mkuu atupe dira ya pamoja kama taifa". Alisema Mongela.
"Pia kwa mkoa wetu wa Arusha hadi sasa kesi zaidi ya 200 za ulawiti na unyanyasaji zimetolewa hukumu na hatua kali zimeshachukuliwa, Kwa gharama yeyote ile tusivumilie vitendo vya unyanyasaji iwe kwa wanawake wala kwa watoto, kuna hatari kubwa sana kama watoto wa kiume kuharibiwa". Aliongeza Mongela.
0 Comments