Na Joseph Ngilisho , ARUMERU
Katibu wa siasa na uenezi wilaya ya MERU ,Kennedy Danford Mpumilwa ameanza kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Samia Suluhu hassañ katika kutangaza utalii wa ndani kupitia hifadhi mbalimbali wilayani humo.
Hii ni baada ya kuwapeleka viongozi zaidi ya 200 wa chama na serikali kutoka kata ya King'ori na maji ya chai kwenda kufanya utalii wa ndani kwenye Hifadhi ya Taifa Arusha ,ARUSHA NATIONAL PARK,(ANAPA) ili kupata uelewa na umuhimu wa kutunza maliasili zetu.
Katibu mwenezi akiwa na viongozi wenzake walifanikiwa kutembelea Hifadhi ya ANAPA akiwa na viongozi hao wakiwemo wanyeviti wa mashina, matawi,na viongozi wa ngazi za kata..
Pamoja na mambo mengine Mwenezi aliwapongeza na kuwashukiru viongozi pamoja na wanachama wa CCM kwa kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wetu na Mwenyekiti wa CCM taifa Dr SAMIA suluhu Hassan ambaye juni 25 aliwahutubia wananchi wa maenwo hayo wakati alikielekea jijini Arusha.
Ends
0 Comments