TAZAMA MIRADI MIZITO YA BIL 10 JIJI LA ARUSHA ILIVYOBAMBA MWENGE WA UHURU ,MKURUGENZI MPYA JIJI AJA NA KAZI MPYA, SHAIB APONGEZA MRADI MZITO CHUO CHA UHASIBU ARUSHA


 

Na Joseph Ngilisho Arusha 


Mwenge wa uhuru kitaifa umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya sekta binafsi na umma katika jiji la Arusha yenye thamani  ya zaidi ya sh,bilioni 10 ukiwemo mradi wa ujenzi wa kituo cha masomo ya uzamili na uzamivu katika chuo cha uhasibu Arusha.


Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Abdalah Shaib Kaim ameeleza kuridhishwa na ubora wa miradi hiyo na kusisitiza kuzingatia matumizi sahihi ya fedha,yanayoakisi uhalisia wa  miradi kwa maslahi mapana  ya taifa .



"Tunafanya ukaguzi wa kina  ili kuhakikisha  kama kweli thamani halisi ya fedha za mradi imetumika "alisema.


Kiongozi huyo wa mbio za mwenge ,aliupongeza uongozi wa chuo cha uhasibu Arusha,kutokana na ubunifu wa kizalendo kupitia ujenzi wa mradi mkubwa wa kimkakati walioufanya.


Naye mkurugenzi wa jiji la Arusha, Jumaa Hamsini, alisema kuwa mwenge wa uhuru unazindua miradi 7 ya kimkakati ikiwemo ya umma na watu binafsi yenye thamani ya sh,bilioni 10.07 ikiwemo miradi ya jiji .



Alifafanua kuwa kati ya miradi hiyo jiji la Arusha linatekeleza miradi yenye thamani ya sh,bilioni 1.2 ikiwemo ujenzi wa barabara ,Nyumba za watumishi ,Mradi wa kuku wa wajasiriamali na mradi wa Soba ,ujenzi wa madarasa na matundu vya vyoo.


"Miradi yote iliyozinduliwa na mwenge imezingatia thamani ya fedha"alisema.


 Awali mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Mrisho Gambo alikipongeza chuo cha uhasibu Arusha,kwa usimamizi bora wa miradi yake na kuzitaka taasisi zingine za serikali kujifunza katika chuo hicho namna ya usimamizi wa kizalendo miradi unaozingatia thamani ya fedha.



Alimpongeza mkuu wa chuo hicho Prof Eliamani Sedoyeka  kwa kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi kutoka 2019 hadi kufikia wanachuo,14,000.


Naye kuu wa chuo hicho Prof Sedoyeka alisema chuo hicho kimefanikiwa kuwa na matawi mbalimbali ikiwemo Babati, Dodoma,Dar es Salaam na tawi jingine linaloanzishwa mjini Songea.



"Chuo chetu kinatakribani wanafunzi 14,000 katika fani za uhasibu ,Tehama, manunuzi,fedha na kimejikita zaidi kuongeza mitaala kutoka  7 ngazi ya shahada kutoka miaka minne iliyopita hadi mitaala 25 ya sasa ukiwemo 17 ya uzamivu .


Ends....

Post a Comment

0 Comments