PROF NDALICHAKO AWASHUKIA VIKALI ,MAOFISA KAZI WANAOTISHA WAAJIRI ILI WAPATIWE RUSHWA,SUALA LA UKIMWI LATAJWA KWA WAAJIRI


 Na Joseph Ngilisho,ARUSHA


WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (KAZi Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu) Prof.Joyce Ndalichako amewaonya vikali baadhi ya maofisa kazi wafawidhi  nchini, wanaotumia vibaya madaraka Yao kwa  kutoa lugha za vitisho, kwa baadhi ya waajiri, wakati wakifanya kaguzi sehemu za kazi,ili wapate rushwa akiwataka waache mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua kali.



Akizungumza  jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa maofisa hao,juu ya kuwawezesha watumishi wanaoishi na Ukimwi na walemavu kufanya kazi bila kunyanyapaliwa, yaliyofadhiliwa na Shirika la kazi Duniani (ILO).


Prof,Ndalichako alisema amekuwa akipokea malalamiko kwa baadhi yao wakitumia vibaya majina ya wateule wa rais kama wametumwa na kutoa lugha za vitisho kwa baadhi ya waajiri jambo ambalo linatia doa kwa mamlaka ya uteuzi.



“Mnapotumia majina ya wateule wa rais mnashusha  hata heshima ya rais aliyetuteua, sasa nimeona leo niwaambie kuanzia sasa nikipata mtu ameenda mahali anatumia jina langu au kamishna wa kazi nitaamrisha akamatwe mara moja na ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria, niwaombe mwache tabia hiyo kwa sababu mtapata tabu kama sijamtuma mtu nikisikia mtapata tabu sana,”alisema


Aliwasihi kubadilika na kutumia lugha za staha wanapotekeleza majukumu ya kazi zao wanapofanya kaguzi kwa waajiri na kuwataka kuacha kubagua kufanya kaguzi kwa waajiri wenye uwezo na kuwaacha wasio na uwezo, kwa kufanya hivyo hakutoi haki sawa kwa wafanyakazi na wanatengeneza mazingira ya rushwa.



Aidha alionya baadhi ya  kauli wanazotoa kwa waajiri hao sio za staha na kuwataka kila mmoja kutumia lugha nzuri itakayomvutia mwajiri kupenda kupata huduma na kwao,  badala ya kutengenenza lugha chafu zinazowatisha na kuwafanya wawe wadogo kama Piritoni na kujikuta wakijengewa mazingira ya kutoa rushwa.


Pia alisema baadhi yao wanafanya kaguzi hewa ambazo hawatoi taarifa sehemu yoyote, badala yake wanaanzisha majadiliano ili kujenga mazingira ya rushwa, ambayo haijawahi kujaa popote na shida haziishi sababu  fedha ikipatikana na matumizi yanaongezeka.



Kadhalika, alionya baadhi yao kuvuka mipaka ya kazi  kwa kwenda kufanya kaguzi eneo ambalo sio lake, na kutolea mfano kwa baadhi yao kutoka Kinondoni kwenda Temeke au Ilala kufanya kaguzi, kitu ambacho hakileti taswira nzuri ya kazi, isipokuwa wanavutwa na waajiri wenye fedha.


Alisema yeye na Katibu Mkuu wake, wamekubaliana samaki mmoja akioza wanamtupa ili asiozeshe samaki wengine, hivyo kila mmoja ajitathimini mwenyewe kabla ya kutupwa nje kutokana na kukiuka misingi ya sheria za kazi.



Aidha, alisema mafunzo hayo anatarajia kuwasaidia  upatikanaji wa haki za wafanyakazi, katika sehemu za kazi na kuondoa ubaguzi na unyanyasaji kwa wafanyakazi hasa wale walio na maambukizi ya Virusi vya Ukiwmi, kwa  kuhakikisha  wanaimarisha kazi za staha na haki sawa kwa wafanyakazi wote.


Naye dokt,George Loy, afisa wa mpango wa umoja wa mataifa wa kupambana na ukimwi (UNAIDC) nchini Tanzania,alisema wamepiga hatua kubwa mapambano dhidi ya ukimwi hapa nchini tangia uingie hapa nchini miaka 40 iliyopita . 



Alisema changamoto bado zipo kwenye maambukizi Mapya na wanaoishi na virusi vya ukimwi namna ya kuwapata ili kuwapatia huduma endelevu na jitihada zinaendelea. 


Takwimu zilizofanywa na serikali na wadau wake wa maendeleo zinaonesha kwamba kiwango cha maambukizi Mapya ni kikubwa kwa kundi la vijana hususani wasichana wenye umri mdogo. 


"Tanzania na nchi zilizo kusini mwa Afrika Takwimu zinaonesha zaidi ya asilimia hamsini ya maambukizi Mapya yapo katika kundi la vijana na wasichana wadogo na hata juhudi za serikali zimeelekezwa kwa kundi hilo ili kukabiliana na kundi hilo"


Naye Mratibu wa masuala ya Ukimwi na usalama sehemu za kazi (ILO) Getruda Sima alisema maofisa kazi,wana uwezo wa kutekeleza sheria na wanauwezo  na nafasi kubwa ya  kutoa elimu kwa waajiri namna ya kuwezesha watumishi wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kufany akazi kwa haki,kukingwa na ubaguzi.



“Mafunzo haya yanawawezesha namna bora ya kutumia  mikataba ya kimataifa, pamoja na mkataba wa  kufanya ukaguzi sehemu za kazi, kwa kuzingatia usimamizi wa haki sawa kwa waathirika wa Ukimwi mahali pa kazi,masuala  ya kijinsia na kusaidia  wafanyakazi walio katika makundi maalum, kama walemavu, ili  kuhakikisha haki zao wanapata  sawa na kutunzwa maslahi yao,”alisema


Ends.... 


Post a Comment

0 Comments