NAIBU WAZIRI AFUNGUA MGODI WA DHAHABU ULIOFUNGWA NA DC, AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUHESHIMU LESENI YA MWEKEZAJI


Na Joseph Ngilisho,Handeni

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameufungua mgodi wa Dhahabu unaomilikiwa na Mwekezaji Mzawa Godfrey Bitesigirwe uliopo  Kijiji cha Kilimamzinga kata ya Kang’ata Wilayani Handeni Mkoani Tanga na kuwataka wachimbaji wasio na leseni kuheshimu mipaka ya leseni za uchimbaji vinginevyo watachukuliwa hatua. 

Mbali ya hilo Waziri Kiruswa alitoa onyo kwa  wachimbaji wadogo wa Madini ya dhahabu kuacha mara moja tabia ya kutorosha madini hayo kwa njia ya panya bila kulipa ushuru wa serikali na kusema kuwa serikali haitawafumbia macho.


Dkt. Kiruswa alisema hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji hicho cha Kilimamzinga mara baada ya kutembelea mgodi huo na kupata maelezo kwa mwekezaji mzawa anayemiliki leseni nane za uchimbaji wa dhahabu na kero za wachimbaji wadogo wasio na lesenileseni na baadaye kuufungua Modi huo kwa maslahi mapata ya mwekezaji na serikali.

 

"Kwanza  kumfungia mwekezaji uliyeingia naye makubaliano nikosa,  anaweza kutushtaki mahalamani au mahalamani za nje ya nchi ukamlipa fidia mamilioni "

Juni 6 mwaka huu ,mkuu wa wilaya hiyo,Albert Msando aliufunga mgodi huo ili kupisha uchunguzi kuhusiana na kuwepo kwa mgogoro baina na mwekezaji na wachimbaji wadogo wasio na leseni wanaotajwa kufikia 4000 ambao wamekuwa wakivamia mgodi huo wa mwekezaji kinyume na utaratibu na kutishia uvunjifu wa amani.


Miongoni mwa madai ya wachimbaji wadogo ni kuitaka serikali kupitia Wizara ya madini kuwapatia leseni zao za uchimbaji ili wawe huru katika shughuli zao tofauti na sasa ambapo wanatumia leseni ya mwekezaji wakidai hawapati uhuru wa kuchimba ipasavyo. 

"Mh naibu waziri sisi tunachoomba serikali itupatie leseni, tunauwezo wa kuchimba na vifaa tunavyo na tutalipa kodi vizuri"alisema Musa Mabawa.

Dkt Kiruswa baada ya kusikiliza kero mbalimbali, alitoa maagizo kwa wachimbaji wasio na leseni kushirikiana na mwekezaji katika shughuli za uchimbaji pia alimwagiza mwekezaji kuweka mdomo wa kuingilia mgodini (Poto)ili kuondoa changamoto ya kuwa na mashimbo mengi yanayoharibu mazingira pamoja na kuepusha mianya ya utororoshaji wa madini. 


Aidha Dkt Kiruswa alitoa onyo kwa askari polisi waliopewa dhamana ya ulinzi eneo hilo kushiriki utoroshaji wa madini kuacha mara moja tabia hiyo kwani inajenga sifa mbaya kwa jeshi hilo.

Aliwataka wachimbaji wadogo kufanya shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo kwa kufuata taratibu za leseni ya mwekezaji.Pia alisema anaheshimu maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando ya awali ya kuufunga Mgodi huo. 


Akizungumzia utoroshaji wa madini ya Dhahabu, Dkt. Kiruswa ametoa anyo kwa wachimbaji wadogo na wafanyabishara wa madini wanaotorosha madini kwa lengo la kukwepa kodi ya Serikali ambapo amewataka kufuata Sheria na Kanuni zilizowekwa na Serikali ikiwemo kuuza madini katika Masoko na Vituo vya Ununuzi wa Madini vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watoroashaji. 

Waziri Kiruswa alitoa muda wa mwezi mmoja kuondoa vibanda vyote vilivyoko katika mgodi huo na kufukia mashimbo ambayo hayatumiki na kuwataka wachimba kupanda miti ili kulinda mazingira.


Naibu waziri alisisitiza kuwa Serikali itamlinda mwekezaji kwa gharama zote kwa kuwa analipa kodi ya serikali ila wachimbaji wasio na leseni watalindwa kwa huruma kwa kuwa ni wavamizi katika mgodi huo na wanatitosha madini.


‘’Serikali haina msalia mtume kwa watoroshaji wa madini ya aina yoyote hivyo basi kwa wale wenye nia ovu dhidi ya madini ya Dhahabu kwa kutaka kujitajirisha haraka haraka na kukwepa kodi ya serikali rungu halitawacha salama’’

Naye Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini John Sallu alimpongeza Dkt. Kiruswa kwa kuumaliza mgogoro uliokuwepo katika eneo la Jimbo  lake ili kuwapa fursa wachimbaji wadogo wadogo wa Dhahabu waweze kunufaika na rasilimali hiyo iliyopo katika kijiji hicho na serikali ngazi zote ziweze kunufaika na malipo ya mirabaha na  kodi.


Sallu ameiomba Wizara ya Madini kutenga maeneo  kwa ajili ya wachimbaji wadogo hususani maeneo yenye leseni ya utafiti yaliyoisha muda wake ili waweze kufaidika na rasilimali madini zilizopo wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya mgodi kufunguliwa , mwekezaji Godfrey Bisitegirwe aliishukuru serikali kwa kufunguliwa mgodi wake na kuahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya mgodi kwa kuweka mdomo mmoja wa kuingilia ndani ya mgodi. 


Mwekezaji huyo ambaye kwa sasa ameajiri wafanyakazi zaidi ya 94 ameahidi kutoa ajira kutoana na uzalishaji na kuahidi kuwa na mahusiano mazuri kwa jamii ikiwa ni pamoja na kutoa misaada pindi anapohitajika kwa faida ya wakazi wa Kijiji kufaidi rasilimali ya madini ya dhahabu.

Alisema atahakikisha anathibiti utoroshaji wa madini ya dhahabu kwa wachimbaji wasiokuwa na leseni wanofanya uchimbaji haramu chini ya mgodi ikiwa ni pamoja na kufukia mashimbo yote ya mtobozano ndani ya mgodi wake kwa wachimbaji hao.

 



Ends...


Post a Comment

0 Comments