Na Joseph Ngilisho,Lushoto
JUMLA ya Miradi ipatayo 17 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2 inatarajiwa kuzinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.
Mwenge huo wa Uhuru unatarajiwa kuwasili katika wilaya hiyo kesho na utazunguka katika halmashauri mbili za Bumbuli na Lushoto Wilayani humo kwa umbali wa km 304.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo,Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Kalisti Lazaro alisema kuwa Mwenge utapokelewa Lushoto kesho Juni 13 mwaka huu katika Kijiji Cha Samata kilichopo Halmashauri ya Bumbuli na utazungushwa katika Halmashauri hiyo kwa umbali wa km 122 na miradi 9 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 779.1 itazinduliwa,kutembelewa na kuwekwa jiwe la msingi
Lazaro alisema kuwa miradi itakayozinduliwa na kufunguliwa katika Halmashauri ya Bumbuli ni pamoja na miradi ya Afya,elimu,maji na barabara na miradi yote imekidhi viwango na imezingatia thamani ya pesa kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi.
Mkuu huyo alisema kuwa Juni 14 mwaka huu Mwenge utapokelewa katika Halmashauri ya Lushoto katika shule ya Msingi ya Kizara na utakimbizwa umbali wa km 173 na miradi 8 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.2 itazinduliwa,kutembelewa na kuwekwa jiwe la msingi .
Alisema miradi itakayozinduliwa katika Halmashauri ya Lushoto ni pamoja na miradi ya Afya, elimu, maji na barabara yenye thamani ya kiasi hicho Cha pesa na miradi hiyo imekidhi viwango na vigezo hususani thamani ya matumizi ya fedha na kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma Kama ilivyowekwa na Serikali.
Lazaro amewataka wà nanchi wote wa Wilaya ya Lushoto na viunga vyake kujitokeza kwa wingi pindi Mwenge wa Uhuru utakapopita barabarani na utakapo kwenda kuzindua miradi ya Maendeleo katika maeneo tajwa katika wilayani hiyo.
Ends....
0 Comments