Na Joseph Ngilisho Arusha
Mpangaji aliyefahamika kwa majina ya Erick Adamu ameuawa kwa kuchomwa na kisu na mpangaji mwenzake Blandina Fred kwa madai ya kushindwa kulipa sh,1000 ya umeme.
Aidha jeshi la Polisi Mkoa Arusha, linamshkilia mtuhumiwa mwanamke, Blandina Fred mkazi wa Kijiji cha IIkirev, Kata ya Olturoto wilayani Arumeru, kwa tuhuma za kumuuwa kwa kumchoma kisu marehemu
Tukio hilo limetokea jana mchana baada ya kutokea ugomvi baina ya wapangaji hao wawili ambapo inadaiwa marehemu Adam aligoma kulipia deni la umeme ambao kwa kawaida wapangaji huchangia.
Wanaomfahamu marehemu wanadai alikuwa msanii wa mziki na shughuli zake amekuwa akizifanyia jijini Arusha.
Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo akizungumzia tukio hilo,alisema lilitokea majina ya mchana wakati, Blandina akiwa na kisu akijiandaa na kupika.
"Kilichotokea ni kuwa wote ni wapangaji walikuwa wakigombana huyu binti alikuwa na kisu kwa kuwa alikuwa jikoni, sasa ndio alimchoma mwenzake,"
Amesema Adam alifariki kutokana na kutokwa na damu nyingi baada ya kuchomwa kisu.
Kamanda Masejo amesema, Jeshi hilo bado linamshikilia kwa mahojiano, mtuhumiwa huyo na bado anahojiwa kuhusiana na tuhuma hizo.
"Taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani kutokana na tuhuma ambazo zinamkabili," amesema kamanda huyo, na kwamba mwili wa Adam umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mountmeru kwa uchunguzi zaidi.
0 Comments