MPUMILWA AWAPIGANIA WAMERU,ALIA NA UBOVU WA BARABARA ,ASIKITISHWA VIONGIZI WA CCM NA SERIKALI KUWA PAKA NA CHUI


 Na Joseph Ngilisho Arusha 

Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM,wilaya ya Meru Mkoani Arusha, KENEDY MPUMILWA amesema kuwa wilaya hiyo bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya ubovu miundo mbinu ya barabara kiasi cha kutishia ustawi wa chama hicho wilayani humo.

MPUMILWA amebainisha hayo katika kikao cha halmashauri Kuu ya CCM Mkoa,wakati mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM Mkoani hapa, katika kipindi cha Januari hadi disemba 2022.


Alisema  yapo maeneo mengi yenye changamoto ya barabara kutopitika hasa kipindi cha mvua,ambapo aliwashauri wataalamu kuhakikisha  wanajenga mifereji ya kupitisha maji ili kuzinusuru barabara   hizo kuharibiewa na maji.

"Mfano barabara ya Kutoka  Pantandi hospitali hadi Akeri juu haipitiki pia barabara ya kutoka Tengeru kuteremka chini zote zimeharibiwa na maji  ya mvua,nashauri wakandarasi wa barabara watengeneze kwanza mifereji ya maji vinginevyo tutakuwa tunapoteza fedha za serikali bura

Kutokana na adha hiyo inayowakumba wananchi wa Meru,bila kupatiwa ufumbuzi MPUMILWA alieleza kuwa chama hicho kinajiweka kwenye wakati mgumu wakati wa uchaguzi kiasi kwamba wananchi wamechoshwa na hali hiyo na kudai wanasubiri tu uchaguzi 2025 wachukue  hatua.

"Ikumbukwe kuwa wilaya ya Meru ni Kordo ya upinzani ,kila mtu anasema subirini mwaka 2025 tutawaonesha jinsi gani watu wanavyoanguka na pikipiki na kufa sababu ya barabara"

Katika hatua nyingine MPUMILWA alidai  katika  wilaya hiyo chama hicho hakina mahusiano mazuri na viongozi wa serikali  na kutaka kuwepo na semina zitakazo  ondoa migongano baina ya viongozi wa kata, kijiji na Mashina wilayani humo.

"Wilaya ya Meru inashida ya mahusiano kati ya viongozi wa serikali na viongozi wa ccm ,ni vema jambo hili nalo likafanyiwakazi ili kurejesha mahusiano kwa mustakabali wa wananchi wetu"


Alisisitiza kuwa hali hiyo ikiachwa iendelee itakuwa na athari kubwa hasa kipindi cha uchaguzi mkuu ujao mwaka 2025.

Ends  ......




Post a Comment

0 Comments