Na Joseph Ngilisho,Mirerani.
Kampuni ya uchimbaji madini ya Gem & Rocky Venture inayochimba madini ya Tanzanite kitalu B katika Mji wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara imetakiwa kuchimba madini hayo kwa kufuata sheria, kanuni na tsratibu waliyopewa na sio vinginevyo.
Hayo yalisemwa na Afisa Mfawidhi wa Madini Kanda ya Mirerani,Mernad Msengi baada ya ukaguzi wa mipaka ya kampuni hiyo na Kitalu C kinachomilikiwa na Mwekezaji Onesmo Mbise kwa kushirikiana na serikali.
Alisema uamuzi wa uhakiki wa mipaka ni kufuatia maamuzi ya rufaa ya kampuni ya Gem & Rock Venture iliyokatwa na Mkurugenzi wake Joel Mollel maarufu kwa jina la Saitoti kutupiliwa mbali na kutakiwa kufuata sheria na kanuni za uchimbaji ikiwa ni pamoja na kurudi katika mgodi wake kama leseni yake inavyosema.
Msengi alisema mbali ya hilo Saitoti ametakiwa kujenga ukuta kutenganisha mgodi wake na mgodi wa kitalu C na kuhakikisha anarudi nyuma hadi eneo lake la uchimbaji.
Afisa Madini huyo ametoa rai kwa wamiliki wote wa migodi ya Tanzanite Mirerani kuheshimu sheria na kanuni za madini pia kuchimba eneo ambalo leseni inaruhusu vinginevyo hatua kali zitachukuliwa ka wale wanaokiuka taratibu kwa makusudi.
Awali kamati maalumu march 28 mwaka huu ilitoa taarifa kuwa Gem & Rock Venture ilifanya makosa katika uchimbaji kwa kuingia ndani ya kitalu C zaidi ya mita 650 na kufanikiwa kufanya uzalishaji wa zaidi ya kilo 4 za madini ya Tanzanite kinyume na taratibu na kufanya uhalibifu hatua ambayo kampuni hiyo ilipinga na kukata rufaa kwa katibu Mkuu wa Wizara hiyo,hata hivyo rufaa ilitupiliwa mbali.
Hata hivyo chanzo cha habari kimedai kuwa ,Saitoti hakuridhishwa na maamuzi hayo na ametishia kurejesha leseni ya uchimbaji ya kitalu B, kwani kilichofanyika ni uonevu dhidi yake.
Ends....
0 Comments