ILANI YA CCM MOTO -RC MONGELA AISOMA KWA SAA 3, APONGEZWA -AFICHUA KILIMO CHA BANGI BALAA!

 


Na Joseph Ngilisho,Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella  amesema  Mkoa wa Arusha unaongoza kuwa kinara wa kilimo cha bangi na wamekamata gunia zaidi ya 6000 za bangi iliyokaushwa wilayani Arumeru na kwenye maeneo ya ukanda wa mlima Meru.


Aidha alisema kutokana na changamoto hiyo mkoa umeanza kuchukua hatua ya kutafuta zao mbadala kwa jamii ya watu wanaolima bangi hiyo sanjari na kutoa  elimu sahihi ya kulima mazao mbadala ili kudhibiti kilimo hicho .

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2022,ambayo iliungwa mkono na wajumbe wote wa mkutano ,Mongella alisema katika kipindi cha miezi sita mkoa huo umepata mafaniko makubwa sana kwani serikali imeleta fedha nyingi  katika mkoa huo



Alisema Mkoa huo katika wilaya za Arumeru na Monduli ndio unaoongoza kwa kilimo cha bangi ukifuatiwa na Mkoa wa Mara na kuongeza kuwa siku nne zilizopita kulikuwa na oparesheni kabambe ya kukamata bangi hiyo na kila nyumba waiyopita maeneo ya Meru ,Kisimiri walikuta magunia ya bangi kavu yakiwa yamepakiwa kwenye nyumba za watu na kufanikiwa kupata magunia 6000 ya bangi


Alisisitiza ingawa zoezi la ukamataji bangi hizo linaendelea lakini serikali inaangalia zaidi wananchi kulima mazao mbadala ili kudhibiti kilimo cha bangi.

"Katika oparesheni tuliyofanya tumebaini maguni ya bangi zaidi ya 6000 yamekamatwa katika oparesheni tuliyofanya hivi karibuni yani wilaya ya Arumeru huko juu kila nyumba ikikaguliwa unakutana gunia la bangi iliyokaushwa "

Alisema kilimo cha bangi kimeshamiri maeneo ya Mlima Meru na baadhi ya nyanda za  maeneo mengine  ya Wilaya yaNgorongoro ya Arumeru na taarifa hizi ni za hadi jana asubuhi.


"Kilimo cha bangi kimeshamiri na gunia zaidi ya 6000 za bangi iliyokaushwa zimekamatwa wilaya Meru katika eneo la Mlima Meru na maeneo ya nyanda za mlima huu"

Alisema pia kunaongezeko la mapato ya ndani na lengo la mkoa ni kila halmashauri zote nchini kukusanya mapato kwa asilimia 100 huku katika sekta ya elimu madarasa 593 yameongezeka na shule za sekondari zimeongezeka kutoka 269 hadi kufikia 272,vyumba vya madarasa 2,851 nakifikia 2,944 Juni mwaka huu.


Alisema Mkoa ulipokea sh,bilioni 10.42 zilizosaidia Ujenzi wa madarasa,huku mradi wa EP4R ukiwezesga Mkoa kupata sh bilioni3,318,600,000 ikiwemo matundu ya vyoo 12 ,mabwei 10,nyumba za walimu,madarasa.

"Kunamaeneo ujenzi unaenda polepole lakini kwenye maeneo ambayo CCM ilifanya ukaguzi ujenzi ulienda haraka lakini mimi niseme Mkuu wa Shule ya Sekondari Sale na Tingatinga wanajitambua sana,hawa wanastahiki pongezi"


Alisisitiza shule ya sekondari Tingatinga ni miongoni mwa shule zinazofanya vema na alitoa rai kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Sale iliyopo wilayani Ngorongoro ni mojawapo kati ya wakuu wa shule anayejitambua na kutekeleza majukumu yake,akiwemo Mkuu wa Shule ya Tingatinga na wengine wengi wapo.

Pia udumavu kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano imepungua ikiwemo kupungua kwa vifo vya kinamama na watoto kutokana na huduma za afya na kusisitiza idadiya vifo hivyo vipungue kabisa.


Mongella alisema changamoto kubwa  iliyopo ni kusimamia miradi ili iweze kwenda kwa wakati hivyo endapo kamati za siasa wilaya na kata zikijipanga vema zinauwezo wa kusaidia chama kusimamia vema miradi mbalimbali.

Alisema ajali za barabarani zimepungua kutoka ajali 69 hadi 40 katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu na kuongeza kuwa ingawa serikali imejenga barabara za lami lakini bado ajali zinatokea.


"Naomba huduma za wazee ziboreshwe zaidi sababu uzee hauna hodi kama umejaliwa umri uzee utakufikia tu hivyo lazima huduma bora kwa wazee ziboreshwe "

Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zelothe Steven alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella kwakuhakikisha Mkoa unakuwa shwari

Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha,Mussa Matoroka alisema vikao vya halmashauri kuu ya CCM vinapaswa kupitia taarifa za utekelezaji wa ilani ikiwemo kuwezesha chama kufanya tathimini ya mambo mbalimbali ikiwemo kukagua miradi inayotekelezwa ili kujirithisha maendeleo yake.


Na endapo kunakasoro zitapelekwa mahali husika kwa hatua zaidi katika halmashauri kuu na alimpongeza ,John Mongella pamoja na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Arusha kwa kusimamia vema na kwenye dosari ni kuelekeza vitu gani vifanyike.

Alimshukuru Mongela kwa kuwaletea wakuu wa idara na vitengo katika kikao hicho cha utekelezaji wa ilani ya chama ambapo utekelezaji huo wa ilani ulihudhuriwa na wenyeviti wa CCM wilaya,wenezi,wajumbe wa chama,wakuu wa wilaya,wakuu wa taasisi mbalimbali za serikali na wakuu wa idara.

Ends...

Post a Comment

0 Comments