COBRA AIBUKA KIDEDEA U-NAIBU MEYA CCM ARUSHA,VERONICA NA BLANDINA WAANGUKIA PUA,MMOJA AAMBULIA SIFURI ,WIKI IJAYO KUCHAGULIWA NA BARAZA LA MADIWANI


 Na Joseph Ngilisho Arusha 

CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Arusha kimemchagua Diwani wa kata ya Kimandolu,Abraham Mollel, (Cobra) kuwa mgombea wa nafasi ya unaibu meya wa jiji baada ya kuwabwaga wagombea wanzake wawili akiwemo aliyekuwa Naibu meya (ccm)Veronica Hoseah, anayemaliza muda wake baada ya kutumikia vipindi viwili mfululizo  aliyekuwa akitetea kiti hicho kwa awamu ya tatu


Kwenye uchaguzi huo wa ndani ya Chama uliosimamiwa na katibu wa Chama cha Mapinduzi, ccm, wilaya ya Arusha, Idd mkowa ,mteule huyo sasa anasuburi wiki ijayo kuchaguliwa kwenye kikao cha baraza la madiwani ambalo lina madiwani kutoka Vyama vya ccm na Chadema ,ambapo Chadema ina Diwani mmoja wa kata ya Olorien 


Kwenye uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi,ccm mkoa, Abraham Cobra, alipata kura 19 huku aliyekuwa Naibu meya diwani Veronika Hoseah akipata kura 11 na diwani Blandina John Makari, akiambulia  sifuli


Msimamizi wa Uchaguzi huo Katibu wa ccm ,Wilaya Idd Mkowa, alimtangaza Abraham Cobra kuwa mshindi na baada ya uchaguzi Baraza la madiwani litamthibitisha Naibu meya huyo mpya ili awe madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja kulingana na kanuni za Tawala za mikoa na Serikali za mitaa {Tamisemi}.


Katibu huyo amewaagiza madiwani kuhakikisha wanaenda kusoma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ili kuwazesha wananchi kuelewa kazi zilizofanywa na utekelezaji wa ahadi za CCM .


Aidha amewataka madiwani hao kuhakikisha wanakuwa na umoja na mshikamano  miongoni mwao na kuachana na makundi  na badala yake wasimamie utekelezaji wa Ilani ya ccm.


Ends....

Post a Comment

0 Comments