By Ngilisho TV-Babati.
Taasisi ya chemchem association ambayo imewekeza katika shughuli za Utalii katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge imetoa vifaa vya michezo kwa timu za wanawake na vijana katika vijiji 10 vinavyounda Jumuiya hiyo
Lengo la kutoa vifaa hivyo ni kushirikisha wanawake na vijana katika uhifadhi kupitia michezo ambayo imeanza katika vijiji hivyo.
Msimamizi wa miradi ya Jamii ya Taasisi hiyo,Nganashe Lukumay akizungumza katika Bonanza la timu za wanawake wa Kijiji Cha Mwada amesema vifaa hivyo vinatarajiwa kuziwezesha timu za wanawake na vijana kujiandaa na michuano ya Kila mwaka ya chem chem CUP.
Nganashe anasema mwaka huu watakuwa na michezo ya Soka kwa wanawake na vijana katika ligi yenye lengo la kupiga Vita ujangili hasa wa Twiga katika eneo hilo.
Amesema taasisi hiyo pia itaendelea kuimarisha kuwajengea uwezo wa kujipatia vipato wanawake kupitia vikundi vyao kujikwamua kiuchumi.
Mwenyekiti wa chem chem CUP,Erasto Belela amesema mwaka huu kwa mara kwanza vijiji 10 vitatoa timu za wanawake na vijana chini ya miaka 18.
"Lengo letu Sasa tunapita vijiji vyote 10 kuhamasisha vijana na wanawake kutumia michezo katika kuendeleza uhifadhi kwani ndio unatupa faida kubwa"amesema
Amesema watarajio ni kuwa vijana na wanawake watakuwa wahifadhi wazuri na Kupambana na ujangili katika maeneo yao.
"Hawa ni chemchem ndio wawekezaji pekee mkoa wa Manyara ambao wanashirikisha Jamii nzima kuendeleza uhifadhi ,michezo na kusaidia huduma muhimu kama za elimu na Afya "amesema
Josephine Pascal mchezaji wa Mwada Qeeen emesema wanapongeza chemchem kwa kuanzisha michezo ya wanawake.
"Sisi tulikuwa hatuchezi lakini tumehamasika kuanza michezo lakini pia tutashirikiana na Hawa wawekezaji kupiga Vita ujangili "amesema
"Mwaka huu kauli mbiu ya michezo ni kuokoa Twiga na tunaimani mwaka huu kutakuwa na msisimko mkubwa kwani na sisi wanawake tumeachia kupenda nyama pori"amesema.
Chemchem imewekeza katika eneo la burunge WMA kupitia Kampuni tanzu ya EBN kufanya uwindaji wa kitalii.utalii wa picha na hotel za kitalii.
Mwisho.
0 Comments