Na Joseph Ngilisho Arusha
Mtu mmoja,Joshua Mashauri (27)Mkazi wa Sekei jijini Arusha,amekufa na mwingine yupo mahututi katika hospitali ya Mkoa Mount Meru, baada ya kugonjwa na basi la Esther Luxury Coach linalomilikiwa na waziri wa fedha Mwigulu Nchemba.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, limetokea jana jioni katika eneo la Sanawari jijini Arusha ambapo watu hao waligongwa wakati wakijaribu kuvuka na mmoja kukanyagwa kichwa na ubongo kumwagika .
Hata hivyo majina ya majeruhi hayakuweza kujulikana mara moja na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali hiyo.
Lakini katika hali isiyo ya kawaida basi hilo baada ya kufikishwa kituo cha polisi liliruhusiwa kuendelea na safari muda mfupi, kinyume na taratibu za polisi zilizozoeleka ,kufanyia uchunguzi tukio kama hilo.
Ends...
0 Comments