TUKIO LA MUME KUMNG'OA MENO NA JICHO MKE KWA PRAIZI MAPYA YAIBUKA MTOTO AFUNGUKA KILA KITU, 'BABA ALIKUWA AKIMPIGA MAMA NA KUMWAMBIA LAZIMA LEO NIKUUE ' RAIS SAMIA ATIA TIMU KWA MAJERUHI ,AAGIZA MAZITO,POLISI YAMNASA MTUHUMIWA AKIWA AMEJIFICHA KWA MCHUNGAJI


Na Joseph Ngilisho Arusha 

Rais Samia Suluhu Hassan  ametoa pole kwa mwanamke,Jackline Mnkonyi (38) mkazi wa Sombetini Jijini Arusha, aliyejeruhiwa vibaya na mumewe ,Isaack Mnyangi kwa kung'olewa meno kwa Praizi na kisha kumtoboa jicho na bisibisi, na kuagiza hatua kali za kisheria zichukiliwe ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.


Salamu hizo za pole zimetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela kwa niaba ya Rais Samia, nyumbani kwa wazazi wa majeruhi huyo eneo la Sinoni, Daraja mbili ,ambapo Mongella alisema Rais Samia amesikitishwa sana na tukio hilo na kuagiza hatua kali zichukiwe ili kukomesha matukio ya unyanyasaji.

"Rais Samia amenituma kuja kutoa pole kwa tukio hili kwa kweli amesikitishwa sana na sisi kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa tumekuja hapa kutoa pole kwa familia na serikali inachukizwa na matukio ya ukatili  na unyanyasaji"


Mongela alisisitiza kwa kuwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi .

Akisimulia tukio hilo mmoja ya watoto wa Jackline, Jensen Mzee alisema kuwa siku ya tukio Mei 23 mwaka huu majira ya usiku akiwa amelala alisikia kelele za ugomvi kati ya mama yake na mtuhumiwa(baba yake).


Alisema alisikia baba yake akimpiga mama yake na kumwambia kuwa leo lazima nikuuwe umezidi umalaya.

"Mimi na wadogo zangu tulikuwa tumelala ila nilishtuka usingizini Nikasikia mama analia huku baba akimwambia leo lazima nikuue ,umezidi umalaya , alimwambia  mama fungua mdomo baadaye mama alinyamaza kimya"

Alisema baba yake aliwafuata chumbani na kuwaambia waamke na waingie kwenye gari na alienda kumvuta mama yao  na kumwingiza kwenye gari na kuwapeleka kwa wazazi wake eneo la Simoni daraja mbili jijini hapa.


Mtuhumiwa Isaack Mnyangi 

"Tulipofika Sinoni majira ya usiku alimteremsha mama na kumwacha hapo  getini kwa babu akiwa hajitambui  na tuliondoka naye kwenye Gari mimi pamoja na mdogo wangu ,ila kesho yake alituleta usiku hapo getini kwa babu na kututelekeza"

Jackline Mnkonyi alioana na mwanaume huyo bila kufunga ndoa akiwa na watoto watatu na alibahatika kupata watoto  wawili na mtuhumiwa huyo .
Jackline Mnkonyi 


Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kumtia mbaroni majira ya usiku, mtuhumiwa huyo akiwa amejificha kwa mchungaji eneo la Himo mkoani Kilimanjaro na kumsafirisha jijini Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa polisi mkoani hapa, Justine Masejo ,mtuhumiwa huyo Isaack Mnyangi (45)alikamatwa jana na polisi wameanza uchunguzi ikiwemo kumhoji mtuhumiwa.


Alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika .

Ends..







Post a Comment

0 Comments