Na Joseph Ngilisho Arusha
JESHI la polisi mkoa wa Arusha limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa ,Isaack Mnyangi (45) aliyemjeruhi kwa kumng'oa memo na jicho kwa praizi na bisibisi Mkewe Jackline Mnkonyi.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Justine Masejo, mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni jana eneo la Himo mkoani Kilimanjaro alikokuwa amejificha kukwepa mkono wa sheria.
0 Comments