TAZAMA #LILIPOFIKIA JENGO LA MAKAO MAKUU YA PAPU, KUZINDULIWA NA RAIS SAMIA,KUBADILI TASWIRA YA ARUSHA,NAIBU WAZIRI ATOA MAAGIZO MAZITO



 Na Joseph Ngilisho, Arusha


Naibu waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhandisi Kundo Mathew amewaagiza wakandarasi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la Umoja wa Posta Afrika(PAPU) unogharimu sh.bilioni 38 kukamilika ndani ya wiki mbili kwa ajili ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan.


Mhandisi  Kundo ameyasema hayo jijini Arusha katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa  jengo hilo ambapo alisisitiza hadi kufikia Juni 20 mwaka huu liwe limekamilika na kuikabidhi serikali kwa ajili ya maandalizi ya ufunguzi huo.

"Wakandarasi mnahitaji muongeze nguvu na mfanye kazi usiku na mchana kutokana na muda wa kukamilisha umeshapita ambapo mradi huo ulipaswa kukamilika machi mwaka huu,"alisema


Amesisitza kuwa ni vyema kazi hiyo ifanyike kwa ubora  kwani kufanya hivyo ni moja ya kulitangaza Taifa pamoja na kujitangaza kibiashara  katika mataifa ya nje kwa kuacha alama ya jengo hilo.

Mhandisi Kundo alisema ni vyema wakandarasi  wahakikishe kila kitu kiwe bora kifikie hadhi ya kimataifa kwani kwa kufanya hivyo ni moja ya kujitangaza kiutendaji kazi.



Aidha alisema kuwa Rais Samia kama kiongozi wa nchi anatekeleza  kazi zake katika kuimarisha mahusiano na Mataifa mbalimbali hivyo ni vyema wakandarasi hao wasimuangushe katika utekelezaji wa mradi huo.

"Aliwataka wakandarasi hao kurekebisha dosari zilizojitokeza kabla ya kukabidhi jengo hilo kwa serikali kwani yeye kama mhandisi atakubali tena kubali kuona aibu ikitokea"



Kwa upande wake Mkandarasi Mshauri wa ujenzi wa jengo hilo,Christopher Sanga alisema maelekezo hayo yaliyotolewa na Naibu waziri yatafanyiwa kazi katika kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati


Jengo hilo limekamilika kwa asilimia 98 na linatarajiwa kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu  Hassan ,Agost 2023.

Awali mradi huo wa gorofa 17 ulianza kutekelezwa mwaka 2018 kwa gharama ya sh,bilioni 38 huku serikali ya Tanzania kupitia mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA ikichangia asilimia 40 na PAPU  asilimia 60.

Ends...


Post a Comment

0 Comments