Na Joseph Ngilisho MONDULI
Watu wanne wakazi wa kijjji cha Jangwani,Mto wa Mbu wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,wanahofiwa kufa wakiwemo wawili wanaodaiwa kupigwa risasi na askari wa mamlaka za hifadhi za Taifa, TANAPA wakishirikiana na polisi wilayani humo.
Akizungumzia tukio hilo mmoja ya wananchi wa kijiji hicho,Samsoni Saria alisema tukio hilo limetokea jana kati ya saa tatu asubuhi na saa 11 jioni katika kijiji cha Jangwani na eneo la Kirurumo wilayani humo.
Alisema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa mipaka kati ya kijiji cha Jangwani ni eneo la hifadhi la ziwa Manyara.
Alisema kuwa jana majira ya asubuhi baadhi ya wananchi wanaojishughulisha na uvuvi walionekana katika ziwa hilo wakivua samaki, ndipo askari wa Tanapa wakiwa na boti ya doria waliwavamia na baadhi yao kuwakamata na kuwafunga pingu .
"Askari wa Tanapa walifika eneo la ambalo baadhi ya vijana walikuwa wakivua samaki wakiwa na mitumbwi ambapo baadhi yao waliwakamata na kuwafunga pingu na wengine waliwatupa kwenye maji"alisema shuhuda huyo.
Tukio hilo liliamsha hasira kwa wananchi wa kijiji hicho baada ya kuwepo taarifa kuwa kuna baadhi ya vijana waliokuwa wakivua ziwani wametoswa kwenye maji wakiwa wamefungwa pingu.
"Ndipo wananchi hao walijikusanya na kwenda ofisi ya kijiji hicho na kufanya uharibifu wakiwatuhumu viongozi wao kupuuza malalamiko yao ya muda mrefu "
Alisema licha ya uharibifu huo wa mali wananchi hao wakiwa wamebeba majani ya miti wakiashilia amani, walienda ofisi za Tanapa zilizopo Kirurumo Mto wa Mbu,na kuwataka askari wa Tanapa wawaonyeshe wenzao wawili ambao hawaonekani.
Hata hivyo askari hao kwa kushirikiana na polisi walifyatua mabomu ya machozi na risasi za moto kwa lengo la kuwatawanya na katika tukio hilo kijana mmoja aitwaye Hasan Adinani maarufu (Saibogi) alipigwa risasi ya kichwa na kufariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya ambapo watano walihamishuliwa katika hospitali ya Rufaa Mount Meru mkoani Arusha .
Hata hivyo katika tukio hilo,mkuu wa wilayaHata hivyo katika tukio hilo,mkuu wa wilaya Joshua Nasary alifika eneo la tukio Kirurumo na kuwasihi wananchi juu ya vurugu hizo.
Katika hali ya isiyo ya kawaida askari haobwaliendelea kufyatua risasi na kusababisha mkuu huyobwa wilaya kukimbia kwa lengo la kijinusuru.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Monduli ,Joshua Nasari alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa mtu mmoja amefariki dunia na wengine kadhaa wamejeruhiwa .
"Tumepata changamoto ya wananchi kujeruhiwa baada ya kutokea sintofahamu kati ya wavuvi wa kijiji cha Jangwani katika ziwa Manyara na askari wa Tanapa na ni kweli mpaka sasa mtu mmoja amepoteza maisha na wawili wamejeruhiwa niwasihi wananchi watulie wakati serikali imashughulikia suala hili "
Kwa upande wake mganga mfawidhi kituo cha Afya Kirurumo,dkt Melisa Saeli alisema wamepokea majeruhu saba wakiwa na majeraha miguuni,tumboni ,befani na kichwani na watano tumewapa rufaa kwenda hospital ya Rufaa Mt Meru,Mkoani Arusha.
Naye Kamishna wa Uhifadhi Tanapa, William Mwakilema akiongea kwa kifupi alikiri kutokea kwa tukio hilo na kieleza kuwa hatua zaidi za uchunguzi zinafanya na jeshi la Polisi ambao ndio watatoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo.
"Ni kweli kuna changamoto imetokea ila tumekaa kikao na kukubaliana kwamba jeshi la polisi wanafanya uchunguzi na ndio watatoa ufafanuzi wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi Mkoani hapa, Justin Masejo kwenda kwa waandishi wa habari,tukio hilo lilitokea maiira ya saa 5.40 katika kijiji cha Jangwani baada ya askari wa Tanapa kuwakamata wavuvi haramu watatu.
Taarifa ilisema kuwa wananchi hao walijikusanya na kwenda ofisi za tanapa zilizopo Kirurumo na kufanya vurugu kubwa kwa kuvunja magari kwa Marungu na Mapanga na kupanga mawe barabarani kuzuia barabarani hiyo kutumika .
Alisema katika tukio hilo mtu mmoja alifariki dunia kwa kupigwa risasi na askari wa Tanapa na uchunguzi wa tikio hilo unaendelea ikiwemo kuwasaka vinara wa vurugu hizo.
Hata hivyo mmoja ya majeruhi aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mt Meru aliyetambulika kwa jina la Athumani Ayubu anadaiwa kufariki dunia.
Wakati huo huo,watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, wakidaiwa kufanya uharibifu katika ofisi ya Serikali ya Kijiji ikiwemo kuchana bendera ya Taifa na kuondoka nayo, huku mmoja akipoteza maisha baada ya ghasia kuzuka baina ya wavuvi na askari wa uhifadhi Tanapa.
.ends..
0 Comments