TAHARUKI MGOMO WA MADAKTARI HOSPITALI YA SELIAN, UONGOZI WADAI HAKUNA MGOMO NI UVUMI TU 'WANACHAPA KAZI'


Na Joseph Ngilisho Arusha 

TAHARUKI imewakumba wagonjwa katika hospitali ya SELIAN Lutheran (ALMC) ya jijini Arusha,kufuatia taarifa za kuwepo kwa mgomo wa madaktari wakiwemo mabingwa wa magonjwa mbalimbali. 

Wafanyakazi hao wanadaiwa kugoma kama njia mojawapo ya kushinikiza kulipwa madai yao ya malimbikizo ya mishahara . 

Hata hivyo uongozi wa hospitali hiyo kupitia mch. Godwin Lekashu na Mkurugenzi wa tiba ,dkt.Frank Madinda umekanusha madai hayo na kusema ni uvumi wa mtaani na Madaktari wote wapo kazini.

MCH.LEKASHU


"Hapa hakuna mgomo, madaktari wote wapo kazini, hata mkiingia huko kwenye vyumba vya madaktari mtawakuta wanachapa kazi"alisema Mch.Lekashu wakati akitoa ufafanuzi ofisini wake.

Alifafanua kwamba  hapa kuwa na mgomo wowote bali madaktari walikuwa na kikao cha kawaida  na uongozi wa hospitali hiyo kilichochukua muda mrefu

Dkt MADINDA

Kwa upande wake dkt Frank Madinda pamoja na kukiri kuwepo kwa wimbi la Madaktari kuondoka katika hospitali hiyo alidai sio kwa sababu ya kukosa mshahara bali ni matakwa yao na haihusiani na changamito za mishahara.

Hata hivyo alisema hospitali hiyo ni tegemeo kwa mkoa wa Arusha na ina madaktari zaidi ya 30 wakiwemo mabingwa bobezi na huduma zake hazijawahi kutetereka .

Post a Comment

0 Comments