RC ARUSHA AZISHUKIA KAMA MWEWE HALMSHAURI TATU KWA KUTOLIPA MISHAHARA WAFANYAKAZI TUCTA YAZICHONGEA ,ATOA SIKU 7 ZIWE ZIMELIPA ,IMO JIJI LA ARUSHA


Na Joseph Ngilisho Arusha 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,John Mongella amezionya baadhi ya halmashauri na kutoa siku saba  kwa halmashauri tatu za mkoa huo ikiwemo jiji la Arusha ,ambazo zimeshindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake kwa muda mrefu na kuwapa usumbufu wa maisha ,kuhakikisha ndani ya wiki moja wanalipa mishahara yao.


Awali mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Mkoa wa Arusha, Lotha Laizer alibainisha  hayo katika maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi mbele ya mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela  kwenye Viwanja vya Sheik Amri Abeid.

Lotta alieleza namna wafanyakazi hao na familia zao wanavyoishi maisha ya tabu kwa kukosa mishahara nanhivyo kukosa huduma muhimu ikiwemo ya afya kwa kutopata mishahara . 

Alisema ipo changamoto kubwa kwa wafanyakazi wanaolipwa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani kwani mishahara yao inachelewa zaidi ya miezi sita haki inayowanyima kupata huduma muhimu ikiwemo za afya.

"Halmashauri sugu kuchelewesha mishahara ya wafanyakazi ni Karatu, Longido na Arusha jiji tunaomba useme nao, sambamba na Halmashauri ya Ngorongoro ambao wao wamekiuka utaratibu wa kulipa zawadi za wafanyakazi bora, ambapo  waliowataja mwaka jana hadi sasa hawajalipwa," amesema.

Lotha alimwomba Mkuu wa Mkoa kufuatilia kwa ukaribu baadhi ya sekta binafsi zinazokiuka muongozo wa Serikali wa kima cha chini cha mishahara na baadhi ya taasisi,kulipa chini ya kiwango cha serikali.

“Hadi leo bado kuna taasisi zinalipa kipato kidogo ambacho hakiendani na mfumo wa maisha wa sasa hasa mfumuko wa bei za huduma na bidhaa mbalimbali kama chakula mbali na hilo baadhi ya waajiri hawataki  kufungua tawi la wafanyakazi katika maeneo yao jambo ambalo ni kinyume na sheria na taratibu hasa wafanyakazi wanapokumbwa na changamoto wanakosa pa kupeleka matatizo yao," alisema.

Akijibu hoja hizo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela ameziagiza Halmashauri za Longido, Karatu na Arusha jiji kulipa mishahara yote ya wafanyakazi wanaodai ndani ya wiki moja kuanzia siku ya leo Jumatatu.

"Mapato yanapokuwa wao ndio wamefanya kazi sasa haiwezekani msiwalipe, naagiza wakurugenzi wa hizi Halmashauri watendeeni haki wafanyakazi wenu ni aibu halimasgauri kama jijinla Arusga kushindwa kulipa wafanyakazi wake kwa wakati.

"Halmashauri ya Ngorongoro acheni utani na haki za watu nataka ifikapo Ijumaa wiki hii nipate uthibitisho wa wale wafanyakazi bora kupewa zawadi zao," amesema.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Katibu wa Tucta Mkoa huo, Abrahamu Kamwela aliwasilisha maombi yao saba mbele ya Mongela ikiwemo kuongezewa mishahara kuendana na ongezeko la bidhaa sokoni, kupunguziwa makato ya kodi ili waweze kupambana na uchumi.

"Mkuu wa mkoa, tunaomba Rais Samia pia atuboreshee huduma za afya lakini pia idhibiti sekta biafsi iendelee kuwapatia bima za afya wastaafu wao kama walivyo wengine wa serikalini, lakini pia tunaomba tume iongeze ofisi kila kanda ili kufanya maamuzi ya rufaa za watumishi," alisema

Baadhi ya wafanyakazi wa halmashauri hizo walidai kuwa hatua ya kucheleweshewa  kwa mishahara yao kuwapata ugumu wa maisha na kussbabisha mianya ya wizi na kumshukuru mkuu wa mkoa kwa kuzishinikiza kulipa stahiki za wafanyakazi hao.

"Kwa kweli tunaishi kwa shida kutokana na mishahara kutopata kwa muda mrefu ila tunamshukuru RC kwa kuliona hilo na kuziagiza tulipwe mara moja "
Ends..

Post a Comment

0 Comments