NEMC YAJIFUA KUPAMBANA NA UINGIZAJI WA TAKA HATARISHI KUPITIA MIPAKANI "HATUWEZI KUKUBALI TANZANIA KUWA DAMOO


Na Joseph Ngilisho Arusha 

Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira nchini,[NEMC] limeanza mkakati wa kupambana na taka hatarishi zinazoingia kupitia mipaka ya nchi na kusababisha athari za kimazingira na afya za kibinadamu.


Akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha, katika  semina ya kuwajengea uwezo maofisa wa serikali  waliopo mipakani, Kupitia mradi wa kujenga uwezo wa kitaifa katika kutekeleza sheria ya usimamizi wa Mazingira juu ya udhibiti wa bidhaa zinazopita mipakani  hasa zenye changamoto ya mazingira.


Mwanasheria Mwandamizi wa NEMC ,Wanjara Kandwa,alisema changamoto ya uingizaji wa taka hatarishi hapa nchini ni kubwa hususani bidhaa za plasitiki ambazo zinaathari ya kimazingira na afya ya kibinadamu na bidhaa  zinazomomonyoa tabaka la ozoni zikiwemo kemikali.


"Tupo hapa kuwajengea uwezo watu wetu waweze kuzisimamia  sheria katika maeneo  ya mipakani wanayofanyia kazi ili kudhibiti bidhaa zinazoingizwa nchini "



Naye meneja wa NEMC kanda ya Kaskazini, LEWIS NZALI alisema kumekuwepo na changamoto kubwa katika uiingizaji na utoaji wa Taka hatarishi kupitia mipaka ya nchi  na hivi karibuni walifanikiwa kukamata shehena ya takataka zikiingizwa nchini kupitia mpaka wa Namanga.


Alisema taasisi hiyo ilifanikiwa kudhibiti takataka hizo na kuamuru zirejeshe katika nchi zilikotoka na hiyo ni kutokana uwezo mkubwa wa wataalamu wa NEMC wenye uwezo wa kubaini usafirishaji wa taka hatarishi.



Alisema kupitia mafunzo hayo maofisa wa NEMC watakuwa na uelewa mkubwa zaidi wa kudhibiti taka hatarishi  kuingizwa kinyemela nchini na kugeuza nchi yetu kuwa dampo la taka. 


"Pia kuna bidhaa zinazotoka hapa nchini bila kibali mfano mapipa ya Lami na aina mbalimbali ya vyuma chakavu ambazo hutolewa nchini kinyemela wakati vyuma hivyo vinahitajika kutumika kama mali ghafi katika viwanda vya ndani"alisema NZALI. 


Ends...








Post a Comment

0 Comments