Na Joseph Ngilisho Arusha
Zaidi ya wachezaji 120 wa gofu kutoka bara zima la Afrika na nje wanatarajia kushiriki mashindano ya wazi ya mchezo wa Gofu yatakayofanyika kwa siku tatu mkoani Arusha.
Mashindano hayo yajulikanayo kama 'Inspire Africa Golf Open,yatachezwa kuanzia Mei 26, 27 na 28 katika viwanja vya Kili Gofu vilivyopo Usa river, mkoani Arusha .
Akizungumza jijini Arusha, mwakilishi wa mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania Mhandisi Enock Magile alisema waliombwa na Festac ambao ni waandaaji wa tamasha la utamaduni Sanaa na michezo linaloendelea jijini Arusha,kuwa wasimamie tukio hilo kutokana na kuwa wao ndio wahusika wa mchezo huo katika kuongoza na kuusimamia .
Magile alisema tukio hilo liko nje ya Kalenda ya taifa ya Gofu ya mwaka lakini wameombwa na waandaaji wa FESTAC kushiriki katika mashindano hayo ya kimichezo ili kuweza kukutanisha wanamichezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Alisema mpaka sasa kila kitu kinakwenda vizuri ikiwa ni Pamoja na zoezi la kujiandikisha likiendelea.
"Ni mashindano ya wazi hivyo wageni waliopo nchini hususani jijini Arusha ni kutoka mataifa mbalimbali ambayo ni Costa-Rica, Marekani, Kenya, Ghana, Uganda, Nigeria, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na Msumbiji,"
Kwa upande wake Mwenyekiti wa FESTAC Mhandisi Yinka Abioye alisema tamasha la utamaduni linalenga kuwakutanisha waafrika kutoka pande zote za dunia ili kuwaweka kuwaweka pamoja kupitia Sanaa/utamaduni na michezo.
Moja ya wadhamini kampuni ya Oryx Energies Tanzania kupitia kwa , Peter Ndomba alisema wao ni wadau wakubwa na wamefanya udhamini kwa Dola za kimarekani 5000...ends
0 Comments