KBC BENKI YAWEZESHA VIJANA 140 KUJIAJIRI ARUSHA, WAKABIDHIWA VITENDEA KAZI VYA MAMILIONI YA FEDHA , RC AIPONGEZA KCB NA GIZ KWA KWA KUWAWEZESHA

 


Na Joseph Ngilisho, Arusha.


Zaidi ya vijana 140 wamepatiwa mafunzo ya muda mfupi na kuwezeshwa vifaa vya kazi ikiwa lengo ni kuwasaidia vijana hao kujiajiri ili kuweza kujikwamua kiuchumu. 


Inaelezwa takribani vijana146 Kati ya 150 wamehitimu mafunzo kutoka chuo cha ufundi (Veta) Oljoro yaliyofadhiliwa na taasisi ya kifedha ya KCB kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la ujerumani Giz kupitia program ya 2jiajiri/E4D vijana hao wamehitimu mafunzo yao na kukabidhiwa vitendea kazi.



Mkuu wa kitengo cha masoko mahusiano na ustawi wa jamii Christna Manyenye amesema taasisi hiyo inampango endelevu unaoitwa 2jiajiri wa kusaidia jamii endelevu na tayari vijana kadhaa wameanza kunufaika na mpango huo.

"Tunafanya kazi y kusaidia jamii yetu na mara kundi likishaingia katika mfumo wa mafunzo haya na benki yetu ya KCB inabaki kuwa mlezi ili kuweza kuwainua kiuchumu,"

Manyenye alisema mradi huo wa 2jiajiri,watu 1780 wamefanikiwa wakiwa ni vijana na wanawake,na mwaka huu waliingiza vijana 5000 na mkakati huo umeshakamilika ikiwa vijana wataanza mafunzo mwezi wa sita mwaka huu.



Mwaka 2016 Hadi 2018 wanawake 315 wamiliki wa biashara ndogondogo walinufaika kwa kupatiwa mafunzo yaujasiriamali na baada ya hapo KCB iliwapatia maafisa watatu kwenda kuwaelekeza katika biashara zao kuhakikisha walichofundishwa darasani  wanakitumia katika biashara zao ili waendelee kupata kipato na kuajiri wengine



Kwa upande wake muhitimu wa mafunzo hayo Rogers Richard mbuguni amesema mafunzo hayo wamepata mafanikio mbalimbali,ujuzi na kutengeneza fedha kupitia kazi wanazozipata mitaani,ajira katika makampuni mbalimbali na kuweza kuwainua kiuchumu.




Mbali na mafanikio hayo vijana hao wameiomba serikali kuwapa kipaombele Mara baada fursa za ajira za mafundi  zinapotokea katika taasisi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na nafasi za jeshi la kujenga taifa JKT kwani wanauwezo mkubwa wa kutumikia nchi. 



Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella amewataka wahitimu hao kuwa na nidhamu ya maisha katika kazi na kuwa na bidii katika kazi.


"Naomba niwaase hasa hapa huko mnapoenda Ile kauli isemayo fundi wa uhakika ni kinyozi pekee isiende kutokea kwenu kafanyeni kazi kwa bidii ili taasisi iweze kunufaika na wewe na kukuhitaji muda wote,"


"Nendeni mkathibitishe kuwa kauli hiyo sio kweli na mafundi wa uhakika wapo,fanyeni kazi tmya viwango na mkachangie kwenye uchumi wa nchi na maendeleo yenu binafsi kwa viwango vya juu,"alisema Mongella.



Mongela aliendelea kuwasisitiza wahitimu hao kwenda kutumia teknolojia vizuri na si vinginevyo,huku akisema kuwa wao kama serikali watarndekea kuwashika mkono katika kila hatua ili kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda.

Ends.....

Post a Comment

0 Comments