KATAMBI AIPONGEZA NACTVET KWA MAONESHO YA ELIMU YA UFUNDI, ATAKA ELIMU YA UFUNDI IWASAIDIE VIJANA KUJIAJIRI


Na Joseph Ngilisho Arusha 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu ,Patrobas Katambi amefunga  maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi jijini Arusha na kusisitiza kuwa elimu ya ufundi inayotolewa katika vyuo mbalimbali hapa nchini iwasaidie vijana kupata ujuzi na kujiajiri ili kujikwamua kiuchumi. 



Akiwa kwenye ufungaji wa maonesho hayo amesema kuwa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanasaidia vijana kupata ujuzi wa kazi mbalimbali za kiufundi na kukuza ajira.



Amewataka washiriki kuendelea kutumia fursa hii hasa vijana kwa kuwa ni sehemu muhimu ya kujifunza na kupata uelewa katika sekta ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.



Naye, Katibu Mtendaji Wa Baraza La Taifa La Elimu Ya Ufundi Na Mafunzo Ya Ufundi Stadi (NACTVET), Dkt. Adolf Rutayuga, amesema kuwa taasisi hiyo itahakikisha inaendelea kutekeleza dhima iliyojiwekea kwa mwaka 2023 ambayo imelenga kuimarisha elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kwa nguvukazi yenye ujuzi nchini.



Alisema kwa sasa NACTVET imejiwekea mkakati wa kuhakikisha elimu ya ufundi yanaleta tija kwa vijana hapa nchini na kuondoa changamoto ya ajira...ends


Post a Comment

0 Comments