Na Joseph Ngilisho Arusha
Maonyesho ya utalii ya KARIBU-KILL FAIR yanayofanyika kila mwaka jijini Arusha, yametajwa kama kichocheo kikubwa katika sekta ya utalii na ni chachu ya kufikia malengo ya watalii milioni 5 ifikapo 2025.
Hayo yamebainishwa na mmoja ya waandaaji wa Maonesho hayo yanayotarajiwa kufanyika jijini Arusha juni 2 hadi 4 mwaka huu,Dominic Shoo wakati akiongea na vyombo vya habari na kueleza kuwa lengo ni kuwaleta karibu watalii kutoka nje ya nchi.
Alisema kupitia maonyesho ya Karibu Kill Fir kila mwaka wageni zaidi ya 500 wamekuwa wakifika nchini kujionea vivutio mbalimbali na nchi zaidi ya 35 zimethbitisha kushiriki.
"Tangu tumeanza maonyesho wageni wamekuwa wakiongezeka kila mwaka hivyo kwa nchi yetu tumekuwa sehemu ya kuchangia pato la taifa" alisema Shoo.
Naye makamu mwenyekiti wa chama cha wasafirishaji watalii TATO,Hendry Kimambo alisema maonyesho hayo ni fursa kwa wafanyabiashara wa utalii kujiuza lakini pia kujua bidhaa mpya za utalii zilizopo sokoni ili kuwavutia watalii wengi zaidi Tanzania.
Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa bank ya CRDB ,Boma Rabilla ambaye alikabidhi hundi ya milioni 50 ikiwa ni sehemu ya mchango wa kufanikisha maonyesho hayo amesema kuna haja ya kuunga mkono jitihada zozote za kuongeza watalii.
"Ikitoka biashara ya dhahabu iliyoingiza Bilioni 2.8 za kimarekani inayofuata ni sekta ya utalii iliyoingiza Bilioni 2.4 hivyo kufanikisha maonyesho haya ni kufanikisha kuongeza fedha za kigeni nchini" amesema Rabilla.
Maonyesho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya magereza katika jijinla Arusha na yatashirikisha wageni mbalimbali huku Makampuni kadhaa kutoka nsani na nje ya nchi yakiwa yamethibitisha ushiriki wake.
Ends....
0 Comments