KANISA LA NABII NAMBA 7 LAPATA USAJILI..MTUME MABOYA ATAKA SERIKALI ICHUKUE TAHADHALI VIONGOZI WA DINI WANAOPOTOSHA WAUMINI YASIYE YAKATOKEA YA KENYA NA KIBWETERE UGANDA


Na Joseph Ngilisho, Arusha 

Kiongozi wa kanisa la CALVARY ASSEMBRY OF GOD ,MTUME DUNSTAN MABOYA ameiomba serikali kufanya uchunguzi wa baadhi ya makanisa ili kujiridhisha na mahubili yanayotolewa na  viongozi wa dini hizo ,kuepuka madhara na imani potofu kama ilivyotokea hivi karibuni katika nchi jirani ya  Kenya ambapo takribani watu 100 wamekufa njaa wakiaminishwa kwenda peponi na viongozi wa dini.



Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki katika ibada ya kumshukuru mungu kwa kanisa la Kingdom of God lililopo Ngaramtoni mkoani Arusha,baada ya kupata hati ya usajili na kulitaka kanisa hilo kuzingatia sheria na taratibu za nchi katika kuendesha taasisi  hiyo.


Aidha alisema kumekuwepo na utitiri wa makanisa yanayoendeshwa bila usajili au kufuata sheria ,hali inayopelekea baadhi ya viongozi wa taasisi hizo  kutoa mahubiri yanayopotosha. 

Mtume Maboya ambaye alikuwa kiongozi wa ibada hiyo na alimpongeza kiongozi wa kanisa hilo la Kingdom Nabii namba 7  kwa kutimiza masharti  na kupata usajili wa kanisa lake ,aliyataka  makanisa mengine kuzingatia  sheria za nchi ili kuepusha kuipotosha jamii kwa mahubili yasiyofaa.



Awali Nabii wa kanisa hilo Mosses Mollel maarufu kwa jina la Nabii namba 7,ambaye pia alitiwa wakfu na kusimikwa kuwa nabii katika tukio lililofanya na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, aliishukuru serikali kwa kumpatia usajili wa kanisa lake na kueleza nia yake ya kufungua matawi ya kanisa hilo katika maeneo mbalimbali hapa nchini. 



Katika hatua nyingine  nabii namba 7 alisema kuwa kanisa lake linashirikiana na serikali katika kupinga mapenzi ya jinsia moja (USHOGA) na kueleza kuwa Jambo hilo linapaswa kupingwa kuanzia ngazi ya familia ,viongozi wa dini na jamii kwa ujumla.


Alisema kuwa lengo la kanisa hilo ni kulitangaza neno la mungu kwa nguvu zote ,ila alikemea utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wanaojiita viongozi wa dini kwa kutoa mahubili yasiyofaa .

Alisema jina la Nabii Namna 7 alipewa na mungu akiwa kwenye maono kama nabii kamili hivyo umaarufu wake umetokana na nguvu ya kimungu aliyonayo katika uponyaji.









Ends...


Post a Comment

0 Comments