Na Joseph Ngilisho Ngilisho Arusha
Huduma ya kanisa la Nabii Namba 7 la Kingdom of God,lililopo Ngaramtoni Mkoani Hapa,huenda ikaenea nchi nzima mara baada ya serikali kuridhishwa na huduma ya kanisa hilo na kulipatia usajili wa kudumu baada ya kutimiza masharti.
Hayo yamebainika katika ibada ya kumshukuru mungu baada ya kanisa hilo kupata usajili ambapo kiongozi wa kanisa hilo Mosses Mollel maarufu kwa jina la Nabii namba 7 , alisema kilichopo mbele yake kwa sasa ni kupanua huduma hiyo iweze kuenea nchini.
"Namshukuru mungu sana kwa kufanikiwa kanisa letu kupata usajili kilichopo mbele yetu kwa sasa ni kupanua huduma zaidi kwa kufungua matawi , halikuwa jambo rahisi sana"
Katika hatua nyingine nabii namba 7 alisema kuwa kanisa lake linashirikiana na serikali katika kupinga mapenzi ya jinsia moja (USHOGA) na kueleza kuwa Jambo hilo linapaswa kupingwa kuanzia ngazi ya familia ,viongozi wa dini na jamii kwa ujimla.
Mbali na shukrani hiyo ,Nabii namba 7 alisimikwa rasmi na viongozi wandamizi wa makanisa mbalimbali washirika na huku kanisa hilo likitiwa wakfu.
Wakati huo huo kiongozi wa kanisa la CALVARY ASSEMBRY OF GOD ,MTUME DUNSTAN MABOYA ameiomba serikali kufanya uchunguzi wa baadhi ya makanisa ili kujiridhisha na mahubili yanayotolewa na viongozi wa dini hizo ,kuepuka madhara na imani potofu kama ilivyotokea hivi karibuni katika nchi jirani ya Kenya ambapo takribani watu 100 wamekufa njaa wakiaminishwa kwenda peponi na viongozi wa dini.
0 Comments