Na Joseph Ngilisho, MONDULI
Mgogoro wa Ardhi ilioamuliwa na baraza la Ardhi na nyumba katika Kijiji cha Lendikinya ,wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, baina ya familia za kifugaji,umechukua sura mpya mara baada ya familia zilizoshindwa katika shauri hilo,kugoma kuachia eneo hilo na kutishia kumwaga damu.
Hali hiyo imemlazimu mkuu wa wilaya hiyo, Joshua Nasary kuingilia kati na kuziamuru pande zote zinazozozana kufika ofisini kwake ili kutafuta namna nzuri zaidi itakayoepusha uvunjifu wa amani unaotishia kuzikumba familia hizo.
Mkuu huyo wa wilaya hiyo amesema anajipanga kutekeleza amri hiyo kwa mlengo mwingine wa amani kwa kuzikutanisha Pande zote na kuangalia namba pekee ya kulimaliza Jambo ila ikishindikana wataacha sheria ichukue mkondo wake.
Uamuzi huo umekuja kufuatia Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya kutoa maamuzi katika shauri la Ardhi namba 125/2007 yaliyompa ushindi, Nakudana Mungaya dhidi ya Yamat Mbaranot na Mbarnot Marmalu wote wakiwa wakazi wa kijiji hicho cha Lendikinya.
Hata hivyo upande wa washindwa tuzo wamepinga kuachia eneo hilo na kuzua taharuki wakitishia kumwaga damu kwa familia ya Mshindi wa tuzo, hali iliyoleta hofu kwa familia hiyo na kuiomba serikali kuingilia kati ili haki iweze kutendeka
Mungaya ,alipata ushindi huo uliotolewa na baraza la Ardhi na nyumba, mbele ya mwenyekiti wa baraza hilo, Fadhili Mdachi, na kuamuru eneo lenye mgogoro lenye ukubwa wa ekari 26 lililopo Moranda katika kijiji hicho ni mali ya Mungaya .
Hata hivyo Mungaya anadai kutishiwa maisha na wanakijiji wenzake walioungana na washindwa tuzo ,jambo liliopelekea ayakimbie makazi yake kwa zaidi ya miezi miwili sasa akihofia maisha yake.
Mkazi huyo ameiomba serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli kuipatia ushirikiano kampuni ya udalali ya Regiz Co.Ltd ya jiji Arusha ili iweze kutekeleza amri halali ya Baraza hilo na aweze kukabidhiwa eneo lake.
Awali baraza hilo lilielekeza kwa amri ya Aprili 2,2023 kuwa washindwa tuzo waondoke wao wenyewe kwenye ardhi hiyo na wabomowe maendeleo yote yaliyowekwa hapo na wakabidhi ardhi hiyibkwa mshinda tuzo ndani ya siku 14 .
"Kwa kuwa amri hiyo bado haikutekelezwa unaamuriwa kuwaondoa kwa nguvu washindwa tuzo na kubomoa maendeleo yote yaliyowekwa na kisha kukabidhi ardhi hiyo kwa mshindwa tuzo ikiwa tupu na kutakiwa kurudisha taarifabkatika baraza hili kabla ya Aprili 17,2023"ilisema sehemu ya maamuzi ya mwenyekiti wa baraza hilo ikimwelekeza Dalali wa mahakama.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha Polisi Monduli, RADEGUNDA MARANDU alisema kuwa jeshi la polisi wilayani humo halijashindwa kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo ila wanachokifanya kwa sasa ni kufanya tathimini namna ya kutekeleza zoezi hilo.
"Sio kwamba tumeshindwa kusimamia utekelezaji wa amri ya mahakama ila tumemwita kwanza dalali wa mahakama ili twende eneo la tukio tukaangalie ukubwa wa zoezi hilo kwa wananchi ili kama litakuwa nje ya uwezo wetu kama wilaya tuweze kushirikisha polisibmkoa kutokana na viashiria vya uvunjifu wa amani kutoka kwa ŵananchi"alisema.
Naye diwani wa kata ya Sepeku ,Sangeti Terutui anayetuhumiwa kuchochea wananchi wasitii amri ya mahakama, alisema kuwa mshinda tuzo amepata haki kiujanja ujanja kupitia vielelezo batili .
Hata hilo alisema hahusiki na kuchochea wananchi kumletea vurugu mshinda tuzo na kusababisha ugumu wa kutekeleza amri halali ya Baraza la Ardhi na nyumba "
Ends...
0 Comments