Na Joseph Ngilisho ,MONDULI
Mkuu wa wilaya mstaafu ,Mathew Sedoyeka amezitaka shule za sekondari hapa nchini kutumia teknolojia za kisasa kufundisha wanafunzi ili kuwajengea uwezo na msingi wa kujiajiri pindi wanapohitimu masomo yao ,waweze kuepuka utegemezi wa ajira za kuajiriwa.
Sedoyeka ameyasema hayo wakati alipohudhulia mahafali ya pili ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Tumaini senior iliyopo Makuyuni,Monduli Mkoani Arusha.Ambapo jumla ya wanafunzi 42 wamehitimu masomo yao na kutunukiwa vyeti.
Pamoja na kuipongeza shule hiyo ya Tumaini Senior kwa kuonyesha njia kwa kutumia elimu ya kisasa ya sayansi na teknolojia kufundisha wanafunzi hao ,alisema ipo haja kwa shule zingine za sekondari nchini kuwajengea msingi imara wa kujiajiri kwa kutukia teknolojia pale wanapohitimu ili kuondoa dhana tegemezi ya ajira serikalini.
"Hapa naomba nisisitize kuwa dunia ya sasa haiwezi kwenda bila teknolojia za kisasa katika sekta mbalimbali ya viwanda, kilimo,ufugaji na biashara na hii lazima shule zetu zifundishe wanafunzi teknolojia katika kuinua uzalishaji "
Alitoa wito kwa shule zingine binafsi au za serikali hapa nchini kwenda katika shule hiyo kujifunza na kuiga teknolojia zinazotumika kufundisha wanafunzi ili kuwajengea msingi wa kujua teknolojia mbalimbali na kutoa rai kwa wahitimu kuitumia vizuri elimu na maarifa walioyapata
Ama katika hatua nyingine alitoa rai kwa shule binafsi kuhakikisha wanafunzi wanafundishwa maadili mema ili kuwaepusha kutumbukia kwenye mila za mataifa ya kigeni jambo litakalo changia kuharibu utu wa Mtanzania.
Awali mkurugeni wa Shule hiyo,Modesti Bayo alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika mchepuo wa masomo ya sayansi na teknolojia kutokana na shule hiyo kujikita zaidi katika elimu ya ufundi tangu mwaka 2016.
Wakati serikali ipo mbioni kufanya mabadiliko ya mitaala ya elimu hapa nchini yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni ,alisema shule hiyo imekuwa ikitoa masomo hayo ya sayansi na teknolojia ambayo yamewasaidia wahitimu kuwapa ujuzi wa kitaaluma.
Alisema shule yake ambayo imejengwa katika jamii ya kifugaji ya kabila la maasai,imesaidia sana kuibadilisha jamii hiyo kupenda kuwasomesha watoto wao na kuachana na dhana ya kuwapeleka kuchunga ili kuwarithisha mifugo.
Bayo amewaita wanafunzi kujiunga na masomo ya kidato cha tani yanayotarajiwa kuanza mapema julai mwaka huu ili kunufaika na teknolojia za kisasa zinazofundishwa na walimu mahili shuleni hapo.
"Shule yetu tunatoa masomo ya ziada ya sayansi na teknolojia, uhandisi tangu mwaka 2016 tunatoa elimu ya ufundi na imekuwa ikifanya vizuri sana na tunawakaribisha wanafunzi wa kidato cha tano kuanzia mwezi wa saba mwaka huu"
Naye mkuu wa shule hiyo, Sifael Msengi alisema mahafali hayo ni ya pili tangu kuanzishwa kwa shule hiyo na wanafunzi wapatao 42 wamehitimu wakiwemo wakike 21.
Alisema matarajio wa wahitimu hao ni kufika ngazi ya vyuo kwani shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kiwilaya ,mkoa na Taifa na wanatarajia wahitimu wote watafaulu vizuri.
Alisema shule hiyo imekuwa ikifundisha elimu ya teknolojia kwa kutumia stadi za ujuzi ili kumfanya mtoto aweze kuiva kwa elimu ya kujitegemea na pindi atakapohitimu masomo asikimbilie kuajiriwa bali akatumie ujuzi alioupata kwenda kujiajiri
Ends.....
.
0 Comments