Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Makamu wa Rais , Dkt Philip Mpango amezitaka Taasisi za fedha na mabenki nchini kutoa mikopo ya riba nafuu kwa makundi mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini,wavuvi, wakulima na wafugaji ili waweze kupiga hatua kujenga uchumi wa taifa.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akifungua mkutano kwa wanahisa wa benki ya CRDB unaofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Aicc jijini Arusha.
Alisema kuwa,taasisi n noyingi za fedha zimekuwa zikitoa mikopo ya riba kwa asilimia 9 ,hivyo aliomba kupunguza zaidi chini ya asilimia 9 ili kuwapa fursa wafanyabiashara wadogo na wananchi waliopo vijijini kuweza kupata huduma za mikopo yenye riba nafuu
.
Aidha ameyaomba mabenki kuongeza bidii katika kupeleka huduma za kibenki vijijini ili kuwapa fursa wananchi waliopo eneo hilo kupata huduma hiyo kwani hivi sasa ni asilimia 8.6 ya wananchi waishio vijijini wanaopata huduma za kibenki hapa nchini.
"Baadhi ya mabenki yanakopesha kwa asilimia 9 hivyo yanapaswa kupunguza zaidi ili kuwapa fursa wananchi wa kipato cha chini hasa vijana na wanawake kuweza kukopa na kujikwamua kiuchumi".
Aidha ameyataka mabenki kubuni madirisha maalumu ya mikopo kwa vijana na wanawake ambayo ni sehemu kubwa ya nguvu kazi ya Taifa lakini bado huchukuliwa kama soko gumu kwa huduma za fedha .
Ameyataka mabenki kuzingatia ufanisi katika utendaji kazi ikiwemo kuongeza gharama za uendeshaji katika matumizi ya Tehama , sambamba
na kuhakikisha hakuna mikopo chechefu mipya na kuzingatia ukomo wa asilimia 5 uliowekwa na benki kuu ya BOT.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya benki ya CRDB, Dkt Ally Laay ameomba serikali kupitia wizara ya elimu kuandaa mitaala maalumu ya kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa kuwekeza katika Hisa ili kuwapa elimu ya fedha wakiwa na umri mdogo.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwekeza kwenye hisa kwani Hadi sasa Taifa lina mwako mdogo sana ya uwekezaji katika maswala ya Hisa
"Bado kuna ufahamu mdogo kwa jamii katika maswala ya Hisa na uwekezaji WA fedha , pendekezo letu ni kuwa tuna haja ya kufundisha somo la mitaala kwenye shule zetu ili vijana wapate ufahamu wakiwa wadogo jambo ambalo litaleta fikra chanya katika uwekezaji wa maswala ya Hisa."amesema.
Awali Mkurugenzi wa benki ya CRDB, Abdulmajjid Nsekela alisema kuwa utaratibu waliojiwekea WA kila mwaka kutoa semina kwa wanahisa umeingeza hamasa kwa wananchi kununua hisa katika Benki hiyo.
Alisema idadi ya wanahisa hapa nchini waliojiunga na mabenki ni chache kwa mabenki mbalimbali kutokana na kutokuwa na elimu ya fedha ndio maana kumekuwa na utaratibu wa kutumia semina ya wanahisa.
"Watanzania tupo zaidi ya milioni 60 lakini ukiangalia kwenye mabenki yote nchini wateja hawazidi milioni 10 wenye akaunti na hiyo ni kutokana na elimu ndogo ya fedha ndio maana benki hii imeamua kufanya maboresho ya kuwa na semina ya wanahisa jambo lililosaidia kuongeza idadi ya wateja wa benki hiyo"alisema.
Alisema wanahisa WA Benki hiyo wanatarajia kunufaika na gawio Nono la asilimia 45 kwa kila hisa tofauti na mwaka jana lilikuwa ni asilimia 35 na hiyo ni baada ya Benki hiyo kupata faida ya sh,bilioni 365 baada ya Kodi.
Ends.....
0 Comments