BENKI YA NMB WADHAMINI WAKUU MKUTANO WA ALAT ARUSHA UAMWAGA MAPESA YAWAANDALIA PATI YA KUKATA NA SHOKA WADAU WAOGELEA VINYWAJI

 


Na Joseph Ngilisho Arusha

 Benki Aya NMB imedhamini kiasi cha Sh200 milioni kufanikisha mkutano wa 37 wa ALAT, unaoanza leo Jumatatu Mei 29 hadi 31 jijini Arusha katika Ukumbi wa mikutano wa AICC.

NMB imechangia kiasi cha Sh200 milioni kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya mkutano huo mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT) unaotarajiwa kufanyika kwa siku tatu mkoani Arusha.

Ofisa mkuu biashara kwa wateja wakubwa na serikali kutoka NMB, Alfred Shao (wa kwanza kutoka kushoto) akikabidhi mfano wa hundi wa Sh200 milioni kwa Makam Mwenyekiti wa ALAT, Sima Costantine (wa kwanza kulia) wengine ni Mkuu wa kitengo cha biashara ya serikali wa NMB Vicky Bishubo na anaefuata katikati ni Kaimu meneja NMB kanda ya kaskazini Praygod Mphuru.


 Mkutano huo umeanza leo Mei 29 hadi 31 kwa kaulimbiu 'Uboreshaji wa miundombinu ni chachu ya utoaji wa huduma bora katika mamlaka za serikali za mitaa' unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC, unafunguliwa na Makamu wa Rais,Dk Philip Mpango.

Akikabidhi mfano wa hundi ya mchango huo, Afisa Mkuu biashara kwa wateja wakubwa na serikali kutoka NMB, Alfred Shao alisema wataendelea kushirikiana na ALAT kulihudumia Taifa kama walivyofanya kwa miaka saba iliyopita ambapo wamekwisha kutoa kiasi cha Sh1.2 bilioni.

"Benki ya NMB tumekuwa na ushirikiano kwa miaka saba tukifadhili jumla ya Sh1.2 bilioni  kufanikisha mikutano yao, na walipokuja tena hatukusita kuwapa tena milioni 200 kufadhili mkutano huu wa mwaka 2023," amesema.

Alisema kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na ALAT hasa katika kutumia mifumo iliyo bora kwenye kuhakikisha serikali inakusanya mapato yake ambayo ndio msingi wa maendeleo serikalini pia kutanua huduma  kwa kufungua matawi 227 nchi nzima ili kufikia hadi wananchi wa chini.

"Sisi ndio tulikuwa benki ya kwanza kujiunga na mfumo wa kieletroniki katika kukusanya mapato ya Serikali na tangu kujiunga NMB imekusanya zaidi ya trilioni 8.6 na tunaendelea na ushirikiano huu uliofanikisha kuunganisha zaidi ya taasisi 1,100 za serikali," amesema.


Akipokea hundi hiyo, Makamu Mwenyekiti wa ALAT, Sima Costantine, aliishukuru NMB kwa kudhamini mkutano wao na ushirikiano mkubwa kwa serikali katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo hususani sekta ya elimu na afya.

"Udhamini wenu kwetu kwa miaka saba ni kielelezo tosha kuwa tumekuwa imara na tunashukuru kwa sapoti hii na tunaomba muendelee hivi hivi kutushika mkono katika halmashauri zetu, serikali za mitaa na serikali kuu," amesema.

Alisema kuwa mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 500 kutoka katika halmashauri 184 nchini.

Miongoni mwa mambo ambayo NMB imefanya ni pamoja na kudhamini  chakula cha jioni (cocktail)katika hoteli maarufu ya kitalii ya Mount Meru.Ambapo wadau walisindikishwa na mziki mzito wa kukata na shoka  na kuserebuka na kufurahia maisha kwa muda na kusahau shida zao.
.ends...

Post a Comment

0 Comments