Na Joseph Ngilisho
MAHAKAMA ya Rufaa ya majaji watu, Tanzania leo imetupa Rufani ya SHARIF MOHAMEDY na wenzake waliokuwa wakipinga adhabu ya kifo kwa kosa la kumuua bilioni ERASTO MSUYA na imemwachia huru dereva wa Sharif,Musa Mangu.
Akiongea kwa niaba ya ..familia ya MSUYA muda mchache baada ya hukumu hiyo,ANTUJA MSUYA alisema wameridhishwa na maamuzi hayo na wanaishukuru mahakama kwa kutenda haki.
Wakati huo huo mmoja wa watuhumiwa wa kosa la mauaji ya mauaji ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, Erasto Msuya maarufu kama Bilionea Msuya, Musa Juma Mangu ameshinda rufaa hukumu ya mauaji hayo, huku wenzake wanne wakikwama mahakamani.
Dar es Salaam. Mahakama ya Rufani imetengua hatia na adhabu ya kunyongwa dhidi ya Mussa Juma Mangu aliyekuwa amehukumiwa kunyongwa, yeye na wenzake wanne, kwa mauaji ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, Erasto Msuya maarufu kama Bilionea Msuya.
Mahakama hiyo imetengua hatia na adhabu hiyo dhidi ya Mangu kufuatia rufaa waliyoikata Mangu na wenzake wakipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowatua hatiani na kuwahukuku adhabu hiyo.
Hukumu hiyo imesomwa leo Jumatano, April 12, 2023 na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Habert George, kwa njia ya video conference, huku warufani hao wakisikiliza hukumu hiyo wakiwa katika Gereza la Ukonga wanakohifadhiwa.
Mahakama yakataa kupokea video kesi ya mke wa Bilionea Msuya
Kitaifa 1 hour ago
Maelezo mke wa bilionea Msuya anavyodaiwa kumuua wifi yake yasomwa mahakamani
Kitaifa 1 hour ago
Mahakama hiyo imetengua hatia na adhabu dhidi ya Mangu baada ya kuridhika kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kumtia hatiani kwa kosa hilo na ikaamuru aachiliwe huru mara moja kutoka gerezani alikokuwa.
Hata hivyo, wakati mahakama hiyo ikimfutia adhabu Mangu na kuamuru aachiliwe huru mara moja, imeamuru wenzake wanne waendelee na adhabu hiyo baada ya kuridhika kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani kwa kosa hilo kama walivyohukumiwa na Mahakama Kuu.
"Rufaa dhidi ya mrufani wa pili Mussa Juma Mangu, imekubaliwa na mahakama hii inaamuru mrufani wa pili, aachiliwe mara moja kutoka gerezani. Warufani wengine wote rufaa yao imekataliwa," amesema Naibu Msajili huyo akihitimisha hukumu hiyo.
Wengine waliokuwa wamekata rufaa hiyo kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, ambao wamekwaa kisiki ni Sharif Mohamed Athuman, Karim Issa Kihundwa, Sadick Mohamed Jabir na Ally Mussa, maarufu kama Majeshi.
Msuya aliyekuwa akimiliki vitega uchumi kadhaa jijini Arusha, aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) Agosti 7, 2013 eneo la Mijohoroni wilayani Hai.
Julai 23, 2018, Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, katika hukumu iloyotolewa na Jaji Salma Maghimbi, aliyeshikilia kesi hiyo, iliwatia hatiani washtakiwa hao watano na kuwahukumu adhabu hiyo.
0 Comments