RAIS SAMIA AMTENGUA MKURUGENZI WA JIJI CHAP,AHUSISHWA NA BIASHARA YA BILIONI MOJA KINYUME CHA UTARATIBU


Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sekiete Selemani.



Bila kutaja sababu za kutenguliwa kwa Sekiete, taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari imesema ametenguliwa tangu Aprili 16, 2023.


Januari 13 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima alimshtaki Sekiete Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni.

Sekiete Selemani aliyekuwa DED MWANZA


Siku hiyo pia Malima aliagiza watumishi wanne wa jiji hilo kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za uuzaji wa viwanja hivyo namba 194 na 195 vilivyopo Mtaa wa Rwegasore jijini Mwanza.


Alidai watumishi hao wa umma wameuza viwanja hivyo vilivyopo mtaa wa kibiashara katikati ya jiji kwa thamani ndogo kulinganisha na bei ya soko.


Huku, Sekiete akidaiwa kukiuka maagizo ya kamati ya ulinzi Wilaya ya Nyamagana na ofisi ya mkuu wa mkoa ya katazo la kurejesha au kufanya uwekezaji wowote wa viwanja vitano kuanzia namba 191 hadi 196 bila kamati hiyo kufahamishwa.


“Kwa mamlaka yangu nimeelekeza ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Mwanza iwasimamishe kazi watumishi wanne ambao ni wakuu wa idara kupisha uchunguzi na tunaandika barua ofisi ya Rais (Tamisemi) kwa hatua kuhusu mkurugenzi wa Jiji,”alisema Malima wakati akizungumza na waandishi wa habari Januari 13, 2023

Post a Comment

0 Comments