GAMBO MATATANI KWA MADAI YA KUHUJUMU MKOA WA ARUSHA, ADAIWA KUCHOCHEA KUNDI LA MACHINGA KUANDAMANA USIKU


Na Joseph Ngilisho Arusha 

Mkuu wa wilaya ya Arusha Felisian Mtehengerwa amesema kitendo cha wafanyabiashara wadogo (Machinga) katika jiji la Arusha kuandamana usiku kinachochewa na wanasiasa wenye nia ovu  ya kuihujumu serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na amemtuhumu mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo kuwa kinara wa mpango huo haramu  kwa kisingizio cha kubughudhiwa na Migambo wa jiji.


Akiongea na vyombo vya habari na kutokea ufafanuzi madai hayo ,Mtehengerwa alidai kuwa Jambo hilo linaratibiwa na kuchochewa na wanasiasa kwa lengo la kuichafua serikali  na kuwachonganisha wafanyabiashara hao na serikali yao. 




Alidai upo ushahidi kwamba Gambo amewapeleka baadhi ya viongozi wa machinga bungeni  dodoma kwa lengo la kuwachongea viongozi wa mkoa ili waonekani hawafai kwa kisingizio cha migambo kutesa machinga kwa kipigo

Alimtaka Gambo kuacha siasa za maji Taka kwani uongozi wote wa mkoa unajua jinsi anavyo hujumu kwa kutumia majukwaa ya kisiasa 

"Jana usiku Machinga wameandamana katika katakana ya jiji la Arusha wakidai mwenzao Isaac Sangwa ameuawa kwa kupigo cha Migambo huu ni uzushi na ni mpango mchafu unaochochewa na wanasiasa wachache kwa maslahi yao ili kumhujumu rais Samia Suluhu ,wasitake kutulazimisha tutumie mamlaka yetu tulionayo "


Alisema wao kama viongozi hawawezi kuruhusu Machinga kufanya biashara kiholela wakati walishatengewa maeneo yao .

"Hili ni jiji la utalii hatuwezi kuruhusu Machinga afanyebiashara kiholela hii ni kufukuza watalii kwa sababu ya wanasiasa uchwara wanaoendesha siasa za maji Taka  kusaka umaarufu "

Awali wamachinga wa soko la Kilombero  jijini hapa, waliandamana wakiwa na madai mbalimbali ya kunyanyaswa kwa kipigo,kuombwa rushwa ya ngono na pesa na Migambo wa jiji la Arusha. 

"Naitwa Janet Lema huyo kijana Isack ni mmachinga mwenzetu alichukuliwa na migambo na kupigwa vibaya sana  na hatujui yupo wapi tumekuwa tukinyanyasika kwa kipigo na kuombwa rushwa ya ngono na pesa"

Jitihada za kumpata Mrisho Gambo ili kuzungumzia tuhuma hizo haikuweza kufanikiwa .

Ends...




Post a Comment

0 Comments