DC ATAKA JIJI LA ARUSHA KUBUNI MIRADI NA KUONGEZA MAPATO YA NDANI...MKURUGENZI TUNAMPANGO WA KUKICHUKUA KIWANDA CHA GENERAL TYRE

 


Na Joseph Ngilisho Arusha 

Mkuu wa wilaya ya Arusha amelitaka Halmashauri ya Jiji la Arusha kuibua vyanzo vya mapato kwa kuandaa mipango mikubwa nakuacha kubweteka na mipango midogo ambayo inasababisha mapato kudumaa.


Aliyasema hayo kwenye kikao cha 25 cha baraza la madiwani jiji la Arusha ambapo aliwataka kuchangamkia fursa mbalimbali katika sekta ya Utalii ambao umeongeza idadi ya watalii nchini.

Alisema kwamba baraza hilo lina mamlaka makubwa ya kusimamia vizuri miradi ya maendeleo kwa kuangalia faida ya Jiji la Arusha na wananchi wake.

Alisema baraza hilo lifikirie kwa mapana vyanzo vipya vya mapato endelevu ikiwemo kuanzisha viwanda ili kunufaika na watalii kwa kubuni miradi ya maendeleo kwa faida ya jiji la Arusha

"Tuache kuongelea masuala ya baraza nje ya vikao tuje kuongelea ndani ya baraza tujadili kwa maslahi mapana ya jiji letu"


"Naombeni sana tuchangamkie fursa za ujio wa watalii kwa kupanua vyanzo vyetu vya mapato, tusijifungie sana ofisini jiji tunamamlaka ya kufanya biashara  "

"Nimeongea na Waziri wa Maliasili na Utalii Mohammed Mchengerwa ameniambia kwa mwaka huu watalii wameongezeka hadi kufikia milion 1.7 hii ni faida kubwa kwa Jiji la Arusha hii"alisema 


Katika hatua nyingine ameliagiza jiji la Arusha kuhakikisha wafanya biashara wadogo (Machinga), wanafanyabiashara zao kwenye maeneo maalumu yaliyotengwa na jambo hilo lisitumike kisiasa sababu Jiji la Arusha ni la Utalii linahitaji ustaarabu.

Alisema  wapo wanasiasa wanaotumia suala la machinga kama mtaji wa kujijenga kisiasa kwa kuwarubuni wafanyabiashara na kuwapeleka maeneo yasiyoruhusiwa.

Kwa upande wa mkurugenzi wa jiji la Arusha,Hargeney Chitukuro alisema kuwa jiji limejipanga kujenga na kuboresha  miundo mbinu ikiwemo masoko pamoja na machinjio ya Arusha meet na kiwanda cha Matofari.


Alisema kuwa masoko yote ya jiji la Arusha yametengewa kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya ukarabati yaweze kuingiza wafanyabiashara wengi zaidi na hivyo kuongeza mapato

Mkurugenzi alisema mpango mwingine ni  kukichukua  kilichokuwa kiwanda cha kutengeneza matairi cha General tyre na kuzalisha matairi.

"Kwa sasa tunafikiria kuomba nankulichukua kiwanda cha General tyre tuweze kuwekeza na kuzalisha matairi maana uwezo huo tunao".

Ends..


Post a Comment

0 Comments