ARUSHA YATISHA KWA USHOGA ,4000 WANARUHUSU KUINGILIWA ,DC ATAKA WANAUME NA WATOTO WAKAGULIWE


Na Joseph Ngilisho, Arusha 


Mkuu wa wilaya ya Arusha Felisian Mtehengerwa ameliambia baraza la Madiwani kuwa hali ya ushoga kwa jiji la Arusha ni mbaya kwani inakadiriwa takribani vijana 4000 wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kuwataka ma

Ameyasema hayo wakati akizungumza katika kikao cha 25 cha baraza la madiwani halmashauri ya Jiji la Arusha mapema leo  jijini Arusha na kuwataka madiwani kupiga vita vitendo hivyo katika maeneo yao.


Aidha ameeleza baadhi ya maeneo ambayo yanatajwa kushamiri kwa vitendo hivyo ni shule za awali (Day care)na baadhi ya taasisi za kijamii (NGOs) ambazo zinaomba usajili kwa minajili ya kutoa elimu kwa jamii.

Alisema taarifa alizonazo kuna taasisi zengine zinakuja kwa mgongo wa kutoa elimu kwa wananchi kumbe zinakuja kuratibu masuala ya ushoga kupitia shule za awali na katika vituo vya taasisi zao.


Akielezea zaidi Mkuu huyo wa wilaya amesema baada ya kufuatilia Mtu huyo ambaye teyari wanamshikilia akwa kusajili taasisi kwa minajili ya kutoa elimu ya ushoga.

"Ukiambiwa idadi ya mashoga hapa Arusha utashika kichwa,kwani ni zaidi ya vijana 4000 kwa takwimu alizonazo huyo aliyekamatwa na wengi ni watoto wetu hivyo hali ni mbaya tuchukue hatua za udhibiti mienendo yao.

Kwa mujibu wa mkuu huyo kuna fedha nyingi zinatolewa kwa shule binafsi na taasisi za kijamii kuratibu na kufundisha mapenzi ya jinsia moja ambapo ukiwauliza wanadai wanatoa elimu ya watu hao kutambua hali zao.

"Juzi kuna mtu moja alibainika kusajili taasisi ya kijamii tulipoifuatilia tumegundua kibali amedanganya na pia taasisi hiyo inajihusisha na vitendo vya kuwafundisha vijana mapenzi ya jinsia moja"

Akawataka madiwani hao kuchukuwa hatua za kukemea vitendo hivyo kwa kuongea na wananchi wa maeneo yao ili kuwafuatilia matendo ya watoto wao wanapotoka na kurudi majumbani mwao.

"Niwaombe wazazi fuatilieni mienendo na muwakague wanaume zenu na watoto wenu hali ni mbaya haiwezekani Mtoto anatoka hovyo bila kuaga na kurudi mzazi hujui mienendo yake hili hata sisi kwenye makuzi hatukulelewa hivyo"

Alisema wazazi wetu walifuatilia mienendo yetu ndio maana vitendo viovu havikuwepo kwa kasi kama sasa kwani kila siku tunapata ripoti ya watoto wawili kulawitiwa.

Alisema tumeshaanza mapambano ya kukabiliana na vitendo hivyo naomba madiwani ushirikiano wenu kwenye mapambano hayo kwani fedha kwenye ushoga ni nyingi sana wakati tuna mambo mengi ya miradi ya maendeleo.

Ends....

Post a Comment

0 Comments