Na Joseph Ngilisho Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela anatarajiwa kuzindua kituo cha Radio cha kanisa la Zion City Tanzania kitakachosaidia kupanua wigo wa uhabarishaji ,uelimishaji na uinjilishaji na kuleta manufaa kwa wananchi waliopo katika mikoa ya kanda ya kaskazini .
Akiongea na vyombo vya habari katika kanisa hilo lililopo Njiro jijini Arusha,Kiongozi Mtume wa kanisa hilo,Trice Shumbusho alisema anamshukuru mungu kuona ndoto ya kanisa hilo ikitimia kwa kufanikiwa kupanua huduma kwa jamii kupitia kituo kipya cha radio kitakachojulikana kwa jina la ZION IMPACT FM itakayopatikana kwenye masafa ya 100.1.
Alisema katika uzinduzi huo utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii,utaenda sambamba na utoaji wa huduma za afya bure kutoka kwa madaktari bingwa kutoka hapa nchini na nchi ya Marekani.
"Uzinduzi utafanyika hapa kanisani siku ya jumamosi tarehe 18 kuanzia majira ya saa 9 hadi saa 12 jioni ila huduma za kiafya zitaanza kutolewa kuanzia alfajiri kupitia madaktari bingwa kutoka Marekani na hapa nchini na pia wagonjwa watapata kutibiwa bure na wale watakaohitaji maombi wataombewa"
Alisema kupitia radio hiyo wataweza kuigusa jamii moja kwa moja kupitia mafundisho ya kiroho, pia watakuwa na vipindi maalumu vitakavyotoa elimu ya ujasiriamali ili jamii itoke eneo moja kwenda hatua nyingine ya maendeleo.
"Radio yetu itakuwa ikifundisha neno la mungu na pia tutakuwa na vipindi maalumu kwa jamii ya kufundisha kazi za mikono ili watu watoke kwenye hali ya umasikini na wawe kwenye hali tofauti"alisema.
Naye muumini wa kanisa hilo ,ambaye pia ni afisa muuguzi ,Loveless mbaga alisema tukio hilo la uzinduzi wa radio litaenda sambamba na utoaji wa huduma muhimu za afya kwa wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.
Alisema huduma zitakazotolewa kwa jamii siku hiyo ni pamoja na uchunguzi afya ya MACHO na kupatiwa miwani bure ,Saratani ya shingo ya uzazi kwa akina mama,magonjwa ya ngozi,
kinywa na meno ,magonjwa ya akili na watatoa ushauri kwa akina mama wenye changamoto ya kutopata mtoto.
Ends...
0 Comments