Na Joseph Ngilisho Arusha
WANANCHI wa kata ya Olasiti jijini Arusha, wamelalamikia kusuasua kwa ujenzi wa daraja muhimu la Kimondorosi linalowaunganisha, wakimtuhumu mkandarasi wa mradi huo kutelekeza mradi huo na kutowatengenezea njia mbadala ya kupita wakati mradi umesimama.
Aidha wamedai kuwa tangia Mkandarasi huyo wa kampuni ya ujenzi ya MATASYA aanze ujenzi wa daraja hilo ,wiki tatu zilizopita ,ameshindwa kuendelea huku akidaiwa kukata bomba la maji safi ili kutumia katika ujenzi kinyume na utaratibu na kusababisha baadhi ya maeneo kukosa huduma ya maji safi.
Wakiongea kwa jazba baadhi ya wanachi hao waliojikusanya eneo la mradi akiwemo balozi wa mtaa wa Kimondorosi,Ufahamu Eliya wamemtaka wakala wa barabara mijini na Vijijini ,Tarura kutazama upya uwezo wa Mkandarasi huyo na
ikiwezekana ivunje mkataba naye kwa sababu ameonesha uwezo mdogo wa kazi yake kwa baadhi ya vifaa amekuwa akiazima kutoka kwa wakazi hao.
Naye diwani wa kata hiyo,Alex Martin amedai kuwa hawezi kuona wananchi wake wakiteseka kwa kikosa njia ya kupita wakati Mkandarasi amepewa fedha za mradi huo zinazotokana na kodi za wananchi .
Aidha alisema udhaifu wa mkandarasi huyo umeonekana hasa katika hatua za awali za kumwaga jamvi katika daraja hilo ambapo zege aliyomwaga ni hafifu na imeanza kubompka na kuweka mashimo hatua ambayo imewatia shaka juu ya uwezo wa mkandarasi huyo na kuiomba Tarura ichukue hatua.
Kipindi hiki kilimtafuta Mkandarasi huyo Joseph Kadogoo ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli ambapo alijibu kwa kifupi kuwa yupo ndani ya muda na mkataba wake unaisha Agosti mwaka huu huku qkisisitiza kuwa masuala mengine kuhusu mradi huo aulizwe meneja wa TARURA.
Meneja wa TARURA wilaya ya Arusha Albert Kyando alipotafutwa kuzungumzia malalamiko ya wananchi alidai kwamba mradi huo ulisimama kuendelea kwa muda kwa kutokana na michoro ya awali kuingilia eneo la mwananchi mmoja ambaye alilalamikia hali hiyo.
"Tumelazimika kupitia upya michoro ya mradi huo mara baada ya mchoro wa awali kuonesha daraja hilo likipita kwenye eneo la mwananchi na awali daraja hilo lilikuwa liwe na urefu wa mita 8 lakini tumelazimika kuongeza hadi mita 15 kupisha eneo la mkazi huyo"
Akiongelea madai kuhusu mkandarasi huyo kutengeneza daraja hilo chini ya kiwango alidai kuwa zege inayoonekana kubomoka baada ya kumwagwa itabomolewa baada ya michiro mipya na ujenzi unatarajia kuendelea mapema wiki hii na mkataba wa mkandarasi utafikia ukomo julai 26 mwaka huu.
Ends..
0 Comments