WAFANYABISHARA MAARUFU WA MADINI WAGEUKIA SIASA WAUTAKA U-NEC ARUSHA,KENEDY MPUMILWA ATAJWA


Na Joseph Ngilisho,Arusha


Wafanyabiashara 
 wa Madini ya Tanzanite Mkoani Arusha,Husein Gonga,Justin Nyari na Thomas Munisi ni miongoni mwa Makada 75 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Arusha waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha ,kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Mkoa.


Wengine waliochukua na kurudisha fomu kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Mbunge wa EALA James ole Millya na Kennedy MPUMILWA katibu mwenezi Meru ambao ni miongoni mwa vijana wasomi wanatajwa tajwa kuimudu nafasi hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari ,Katibu wa CCM Mkoa Arusha,Mussa Matoloka alisema fomu zilichukuliwa 84 na Makada wake,wabunge na wafanyabiashara Ila waliorudisha fomu ni wagombea 75 katika Mkoa wa Arusha.
Mfanyabiashara wa madini Justin Nyari 


Matoroka aliwataka  wagombea NEC Arusha kuzingatia maadili ya chama ikiwa ni pamoja na kufuata Kanuni na taratibu za chama na Kamwe chama hakitasita kuchukua hatua kwa mgombea atayetoa rushwa kutaka nafasi hiyo.

Uchaguzi huo ni wa marudio baada ya ule wa Awali kufutwa novemba mwaka Jana na Kamati kuu ya CCM baada ya kuelezwa kuwa baadhi wagombea walionyesha vitendo vya rushwa waziwazi hatua ambayo ni kinyume na maadili ya chama.

Kabla ya kufutwa kwa kinyang'anyiro hicho cha U-NEC Novemba mwaka jana Wafanyabiashara wawili wakubwa jijini Arusha,Gesso Bajuta na Bilionea Sendeu Laizer walionesha umwamba wa kugombea nafasi hiyo.

Hata hivyo zoezi lililokuwa likiendelea leo kwa makada wote waliorejesha fomu ni kuhakiki taarifa zao ikiweno uanachama wao usio na mashaka ndani ya ccm.Wa



Mwisho 

Post a Comment

0 Comments