NEMC YAFUNDA MAKANISA YANAYOPIGA KELELE CHAFUZI..MEYA ATAKA YAFUATE SHERIA ZA MAZINGIRA


Na Joseph Ngilisho Arusha 

MEYA wa Jiji la Arusha ,Maximilian Iranghe amewataka wamiliki wa Makanisa na Misikiti mjini hapa,kufuata  sheria za utunzani wa Mazingira na kuacha kuzalisha  kelele chafuzi zinazobughudhi na kuleta athari kwa wananchi.

Iranghe ametoa kauli hiyo mapema leo wakati akifungua semina kwa viongozi wa dini kuhusu utunzaji wa mazingira,yaliyoandaliwa  na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC na kutaka mafunzo hayo yawe endelevu ili kupunguza athari zinazotokana na mitetemo ya mziki  


Alisema kuwa uchafuzi wa mazingira upo wa aina mbalimbali ikiwemo kelele zinazotokana na baadhi ya wamiliki wa makanisa,kumbi za starehe kushindwa kudhibiti vyombo vyao vya mziki ukizingatia kwamba baadhi ya makanisa yapo ndani jamii . 

Alisema zipo sheria zinazosimamiwa na NEMC  zinazokataza uwepo wa kelele chafuzi zinazobughudhi wengine lakini baadhi ya watu ama kwa kutojua au wanajua lakini wamekuwa wakifungulia mziki kwa kiwango juu. 


"Wenye kumbi za starehe , makanisa na misikiti wazingatie sheria za mazingira na kuacha kubughudhi kwa kufungulia mziki kwa sauti kubwa,watambue kuwa faini zipo na wasimamizi wa hizi sheria wapo kazini"

Awali Meneja wa NEMC kanda ya Kaskazini,Lewis  Nzali alisema wamelazimika kutoa semina hiyo kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya uwepo wa kelele chafuzi zinazosababishwa na makanisa,viwanda,misikiti na kumbi za starehe.


Alisema semina hiyo imelenga kuwaelimisha ili watambue sheria za mazingira na kwamba baada ya hapo watakao kamatwa wamekiuka sheria hiyo watakabiliwa na faini ya sh, milioni tano au kufungo cha miaka saba jela.

"Wapo watu wanaofanya fujo za kelele wakati wakijua ni kosa ila kutokana na pesa zao wamekuwa wakindisha sheria ili watakapo kamatwa walipe faini ila sisi tumejipanga tukiwakamata tunawafikisha mahakamani na kuitaka mahakama iwafunge jela"


Baadhi ya viongozi wa dini,mch.Estomih Mwanga wa kanisa la Last Glorious ,lililopo Ungalimited na Julieth Masawe wa kanisa la Pentekoste Ebenezer walisema semina hiyo itawasaidia sana katika kusimamia mazingira kwani wengi wao walikuwa wakiendesha mahuburinkwa sauti kubwa kwa sababu hawakuwa wanajua kuwa ni kosa kisheria.

"Ki ukweli tulikuwa hatujui kama tunavunja sheria kwa kupiga kelele zinazochafua mazingira ila tulikuwa tunajua ni kwamba tunaendesha ibada kilalali"alisema mch.Julieth.

Naye mch Mwanga alisema semina hiyo ni fursa ya kupata elimu itakayosaidia kuwarejesha kwenye msingi na kuepusha kupiga kelele chafuzi kwenye makanisa yao.

Aliwataka wachungaji wenzake kupokea elimu hiyo na kuipeleka makanisani ili kuepusha uvunjaji wa sheria ya mazingira na kuwataka washiriki vema zoezi la upandaji miti.

Ends....









Post a Comment

0 Comments