MJAMZITO APOTEZA MIMBA YA MIEZI SITA KWA KIPIGO ..HAKIMU AIFUTA KESI YA MTUHUMIWA KINYEMELA ..MCHEZO MCHAFU WATAJWA

Shamila Mohamed aliyepotez ujauzito wa miezi sita kwa kipigo

Na Joseph Ngilisho Arusha 


MKAZI wa mtaa wa mji mpya katika kata ya Olasiti jijini Arusha,Shamila Mohamed (21)amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa kipigo na jirani yake ,Diana Matata na kusababisha  mimba yake ya miezi sita kutoka.

Aidha mkazi huyo amelalamikia hatua ya kufutwa kinyemela kwa kesi iliyokuwa ikimkabili mtuhumiwa huyo katika mahakama ya mwanzo ya Maromboso huku hakimu aliyeifuta akidaiwa kuwatishia kuwasweka ndani ndugu wa mlalamikaji iwapo wataendelea kufuatilia.

Akiongea kwa tabu nyumbani kwake,Shamila ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru,alisema kuwa jirani yake huyo alimvamia nyumbani kwake na kuanza kumshambulia kwa mawe na kisha  kumbamiza kwenye meza hali iliyomsababishia maumivu makali tumboni kwake. 

Alisema mara baada ya tukio hilo alitoa taarifa kituo cha polisi cha Muriet na mtuhumiwa alikamatwa na februali 16 mwaka huu,alifikishwa kwenye mahakama ya mwanzo Maromboso jijini hapa.

"Siku ya tukio nilifikishwa katika hospitali ya Mount Meru nikiwa sijitambui na baada ya kupimwa niliambiwa mtoto wangu amekufa niliumia sana na chaajabu kesi ya mtuhumiwa imefutwa hii sio haki kabisa naomba serikali inisaidie"alisema

Mume wa mlalamikaji,aitwaye Merick Kigahe alisema kuwa mtuhumiwa baada ya kufikishwa katika mahakama hiyo na kusomewa shtaka la kujeruhi,hakimu wa mahakama hiyo,Kasimiri Toto aliweza  kuahirisha shauri hilo hadi Machi 10.
Melick Kigahe mume wa mjamzito


"Tulipofika mahakama hapo siku ya tarahe 10 juzi, tulikaa  kwa muda mrefu bila kuitwa na tulipoona muda umeenda tulienda kumuuliza hakimu ambaye alitujibu kuwa kesi yetu imeitwa  na hamkutokea imefutwa"

Kigahe alisema hawakuridhishwa na majibu hayo na kuwalazimu  kumwomba hakimu huyo kuwapatia ufafanuzi zaidi wa kisheria lakini  aliwajia juu akiwaeleza "mkiendelea kusumbua nitawaweka ndani"jambo lililowafanya waondoke huku wakiamini kuna mchezo mchafu umechezwa.

"Siku iliyofuata niliamua kwenda kumwona   hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo ya Maromboso ambaye alinishauri niende kituo cha Polisi Murieti nikatoe malalamiko yangu "alisema 

Balozi wa mtaa  huo ,Winfrida Mboya alieleza kusikitishwa na hatua ya kufutwa kwa kesi hiyo alidai kuwa mtuhumiwa huyo ameshindikana kwa matukio ya ugomvi wa mara kwa mara hapo mtaani kiasi cha kutishia amani ya wa  nanchi.

"Kuna matukio zaidi ya matano ya huyo mama Peter(Diana) amelalamikiwa na majirani zake na anapokamatwa na kufikishwa polisi huwa nahonga na kutoka , sasa kitendo cha mahakama kufuta kesi yake kimenisikitisha sana"

Akiongelea tuhuma hizo,Diana Matata alikanusha kumpiga Shamila na kusabisha ujauzito kutoka ,akidai kwamba Mimba za Shamila zimekuwa zikitoka kwa sababu mfuko wake wa uzazi ni mwepesi na hiyo ni mara ya pili ,mara ya kwanza ilitoka akiwa amepanga katika nyumba yake.
Diana Matata jirani anayedaiwa kumtoa mimba kwa kipigo mwenzake


"Mimi sikuwa na ugomvi na Shamila ila nilikuwa na ugomvi na dada yake aitwaye  Shamimu kwa sababu alimwambia mwanangu ni shoga "

Kuhusu suala la kufutwa kinyemela kwa kesi iliyokuwa ikimkabili  alidai kwamba hilo ni suala la mahakama hawezi kuiingilia.

Akiongelea sakata hilo hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo ,James Keraryo alisema anafuatilia suala hilo hata hivyo aliwatupia lawama polisi akidai wameleta kesi bila kuwajulisha wahusika .

"ngoja nitaifuatilia, ila polisi ndo wana makosa wanaleta kesi mahakamani bila kuwajulisha walalamikaji, na hakimu anatumia kuiondoa kwa kifungu cha sheria kama mlalamikaji hayupo"alisema James.

Ends










Post a Comment

0 Comments