Na Joseph Ngilisho,ARUSHA
KINYANG'ANYIRO cha kuwania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC )mkoa wa Arusha, kimeanza rasimi leo mara baada ya vigogo kadhaa kujitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo.
Miongoni mwa waliojitokeza ni Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA) James ole Millya ambaye alisema amejipanga vema kukitumikia chama cha Mapinduzi kupitia mkoa wa Arusha katika nyanja za kisiasa.
Mwingine aliyechukua fomu kuwania nafasi hiyo ni Hussein Gonga ambaye alifika kimya kimya na kukabidhiwa fomu na sekretari wa chama ambaye hakupenda kutaja jina lake litajwe baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha,Mussa Matoroka kuwa kwenye ziara ya Utelelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoani.
Millya ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Simanjiro alisema ameona ni vema agombee nafasi hiyo ili kuusaidia Mkoa wa Arusha ambao ni lazima kuwepo na timu imara itakayohakikisha chaguzi zijazo chama kinashinda kwa kishindo.
Alisema yeye kama kijana aliyepikwa na chama amejitoa kuwania nafasi hiyo ili kusaidia chama kushinda kwani anajua vema siasa za nchi ya Tanzania
Alimpongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwakuruhusu mikutano ya Vyama vya Siasa hivyo kutokana nauzoefu wake katika nafasi zake alizokuwa nazo awali anaamini akipata nafasi ya ujumbe wa Halmshauri kuu atakisaidia chama kupata mafanikio na ushindi.
"Ninauzoefu wa kisiasa na naomba ridhaa ya kuwania nafasi hii kwani sifa na uzoefu wa pande zote mbili katika chama ninao"
Uchaguzi huo ambao ulikuwa ufanyike Novemba mwaka jana ulifutwa kutokana na vitendo vya rushwa kwa baadhi ya makada wa ccm waliokuwa wakiwania nafasi hiyo kuoneshana nguvu ya pesa.
Hata hivyo Millya alisema kuwa atakuwa muumini namba moja wa kulaani vitendo vya rushwa ndani ya uchaguzi huo akiamini kiongozi bora hupimwa kwa matendo yake na sio kwa rushwa.
Katibu wa ccm Mkoa wa Arusha,Musa Matoroka alisema zoezi la uchukuaji wa Fomu limeanza leo Machi 23 hadi machi 25 mwaka huu saa .
Alisema wagombea wote waliokuwa wakiwania nafasi hiyo kabla ya zoezi hilo kufutwa wataruhusiwa kuchukua fomu .
Miongoni mwa wagombea waliokuwa wakiwania nafasi hiyo kabla ya uchaguzi huo kufutwa ni pamoja na Mfanyabiashara na mchimbaji wa Madini ya Ruby ,Bilionea Sendeu Laizer na mfanyabiashara wa madawa ya mifugo, Gesso Bajuta .
Ends..
0 Comments