Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Kiongozi wa dini ya Kiislamu,Alhaji dkt. Sulle aliyejipatia umaarufu kutokana na maombezi yake ya kiroho yanayoponya na huduma ya matibabu,ameibuka na kueleza namna alivyofanikiwa kuisaidia jamii kupitia huduma zake.
Akiongea na vyombo vya habari jiji Arusha,dkt Sulle ambaye pia ni Mkurugenzi wa kituo cha Islamic foundation kinachojishughulisha na utoaji wa huduma za maombezi na uponyaji .
Alisema ameamua kutumia mfungo wa ramadhani na mfungo wa kwaresima kwa wakristu kutoa maombi maalumu (DUA)kwa jamii kupitia mahubiri ya mihadhara anayoifanya katika mikoa mbambali nchini ili jamii iondokane na dhambi na kumrejea mwenyezi mungu .
"Dunia kwa sasa imeingia kwenye maasi makubwa ikiwemo ndoa za jinsia moja (ushoga) ,ukatili na mauaji ambayo mwenyezi mungu ameyakataa ,hivyo sisi kama viongozi wa dini lazima tuyakemee kupitia elimu ninayotoa"
Alisema katika kipindi hiki ambacho waumini wa dini ya kiislamu na wakristu wakiwa wameingia kwenye mfungo mmoja wakimwomba mwenyezi mungu ,atatumia fursa hiyo kutoa elimu ya dini na maombi maalumu yanayoponya ili jamii iachane na matendo maovu.
Akizungumzia umaarufu wake kupitia mitandao ya kijamii alisema kwamba amekuwa akifundisha kupitia jumbe maalumu anazotoa kwa jamii ikiwemo kukemea watu waliojificha kwenye dini wakati ni watenda maovu wakubwa.
Alisema ujumbe mwingine ni tabia za wanaume wanaojifanya wacha mungu kwa kuoa mke mmoja wakati wana matamanio kibao, wanagubikwa na michepuko hali inayosababisha mifarakano kwenye ndoa zao .
"Ukitaka kuona hasira ya mwanaume gusa simu yake kwa sababu simu ya mwanaume ni kama kitunguu maji ukikitazama wakati unakikata lazima kikutoe machozi"alisema Alhaji
Alisema ujumbe mwingine ulioiteka mihadhara yake na kumpatia umaarufu ni pale anapokiwa akidadavua kuwa mama yake yesu ndiyo mwanamke bora zaidi kuliko wanawake wote duniani.
Kuhusu tiba mbalimbali anazotoa kwa jamii alidai kuwa amekuwa na uzoefu wa miaka 30 akifanya tiba mbalimbali kupitia tiba za kiroho,huduma za mimea asili kupitia tafiti mbalimbali pamoja na kutoa ushauri nasaha.
Ends...
,
0 Comments