Na Joseph Ngilisho,Mirerani
Kamati Maalumu ya Wataalamu wa Ramani Migodini kutoka Chuo Cha Madini Dodoma imemamliza Mgogoro kati ya Kampuni ya Madini ya Franone na Gem & Rock Venture na kusema kuwa madini yenye uzani wa kilo 4 yalichimbwa mita 650 ndani ya Mgodi wa Kitalu C unaomilikiwa na serikali na mwekezaji Mzawa Onesmo Mbise yalichimbwa kinyume cha sheria na serikali imeyataifisha.
Mbali ya hilo Kamati imebaini katika uchunguzi wake kuwa mageti ua chini ya mgodi yaliyowekwa na Kampuni ya Gem & Rock Venture inayochimba mgodi wa kitalu B inayomilikiwa na Mkurugenzi Joel Mollel maarufu kwa jina la Saitoti yaliwekwa ndani ya Mgodi wa kitalu C eneo ambalo kampuni ya Saitoti inafanya uzalishaji.
Akiongea ofisini kwake ,afisa Madini Mkazi,Mererani (RMO),Mkoani Manyara,Mernad Msengi alisema kuwa baada ya kamati kubaini hilo, iliagiza Kampuni ya Gem & Rock Venture kuwa mageti waliyowekwa chini ya ardhi yafuate leseni husika na Madini yaliyozalishwa katika eneo la mgogoro yataendelea kushikiliwa na serikali hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
Msengi alisema majibu ya kusudio la kufungiwa mgodi iliyotolewa na Kampuni ya Gem & Rock Venture kwa Wizara ya Madini hayakuiridhisha ofisi yake hivyo mgodi utaendelea kusimamisha shughuli za uchimbaji hadi pale itakaporekebisha kwa ukamilifu makosa yote yaliyoelekezwa na Wizara ya Madini juu ya Ukiukwaji wa leseni uliofanywa na Kampuni hiyo.
Msengi alisema timu hiyo ya Wataalamu ilifanya kazi kwa muda wote ndani ya mgodi kushirikiana na vyombo vyote vya dola katika Wilaya ya Simanjiro{Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Simanjiro}, Viongozi wa Mgodi wa Kitalu C na B na baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Madini lengo ni kutaka taarifa za kiuchunguzi ziwe wazi na huru na kusiwe na kificho ili kuondoa lawama zisizokuwa za Msingi kwa pande zote.
Mbali ya Saitoti kumiliki Kampuni ya Gem & Rock Venture kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mwenza,Sammy Mollel katika Mgodi Kitalu B walituhumiwa kuchimba Bomu katika Mgodi wa Kitalu C mgodi unamilikiwa na serikali na Mwekezaji Mbise na kufanikiwa kutoweka na madini kilo 4 lakini kabla ya kukimbia nayo Maofisa wa Wizara ya Madini Mirerani walifanikiwa kuwapora na kuyahifadhi katika ofisi Madini Mirerani.
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema katika hotuba zake siku za nyuma kuwa wale wote wanaochimba Bomu katika mgodi wa Tanzanite Kitalu C kuacha mara moja vinginevyo dola haitawaacha salama pindi watakapokaidi amri kwani kitalu C ni mali ya serikali na Mwekezaji Mzawa anayemiliki Kampuni ya Uchimbaji ya Franone ya Jijini Arusha.
Hivi karibuni ilidaiwa kuwa wafanyakazi 30 wa Kampuni ya Gem & Rock Venture walivamia mgodi wa Kitalu C kwa njia ya Bomu na kuchimba Madini ya Tanzanite kibabe ndani ya mgodi huo na kufanikiwa kupora Madini ya kilo 4 hayo lakini uongozi wa Kampuni Ya Saitoti ulipinga na kusema kuwa wao ndio wameporwa Madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 6.
Katika hatua nyingine uongozi wa mgodi huo umempiga marufuku mfanyabiashara Saitoti kuingia ndani ya lango la machimbo ya madini ya Tanzanite Mererani kwa sababu ambazo bado hazijafahamika.
"Ukifika kwenye lango kuu la kuingilia ndani ya Mgodi wa Tanzanite utakuta picha za Saitoti na wafanyakazi wake wawili zikiwa zimebadikwa na kuandika hawaruhusiwi kuingia ndani"walisema baadhi ya
wachimbaji.
wachimbaji.
Hata hivyo Saitoti alipoulizwa juu ya taarifa hizo alidai kwamba yupo njiani anatoka Nairobi ,Nchini Kenya hivyo hafahamu chochote kinachoendelea katika Machimbo hayo na kuahidi atazungumza akipata taarifa kamili.
Hivi karibuni mfanyabiashara Saitoti na wenzake 7 walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya Simanjiro mkoani humo akishitakiwa kwa makosa mawili likiwemo la kukiuka amri halali kuhusu suala maelekezo ya uchimbaji.
Hata hivyo Mfanyabiashara huyo na wenzake walikana mashtaka na kuachiwa kwa dhamana hadi Aprili 14 mwaka huu.
Ends...
0 Comments