MENEJA WA MGAHAWA WA KITALII ANASURIKA KUBAKWA,KUPORWA NA KUUAWA,AJERUHIWA VIBAYA 'WALINIVUA SURUWALI'


Na Joseph Ngilisho Arusha 

MEMEJA wa mgahawa wa kitalii wa banana hause uliopo Ilboru Kisiwani,mkoani Arusha, Helleni Simba amenusurika kuuawa na watu wasiojulikana baada ya jaribio la kumbaka na kumwibia kushindikana ambapo walimjeruhiwa vibaya kwa kumkata na kitu chenye ncha kali katika mkono wale wa kushoto na kushonwa nyuzi zaidi ya 30.

Akiongea na chombo cha habari Mkurugenzi mtendaji wa mgahawa huo,Ombeni Parangyo anayeishi  nchini marekani ,alidai kuwa watu hao walimvamia mfanyakazi wake majira ya usiku akiwa chumbani kwake baada ya kufanikiwa kuvunja mlango wa chumba hicho.

Ombeni Palangyo,  Mkurugenzi wa Banana House 

Alisema kuwa watu hao wanaodhaniwa kuwa ni wakazi wa eneo hilo la Ilboru, walifika katika eneo hilo la mgahawa na kukaa kama wateja na baadaye majira ya usiku  walinyanyuka na kumfuata chumbani kwake alikokuwa amelala katika mgahawa huo.

Alidai kuwa baada ya kufanikiwa kuingia ndani walianza kumvua nguo na wakati akijaribu kujitetea walimpiga ngumi za usoni na kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali kwenye mkono wake wa kushoto ambapo alianza kipiga kelele ndipo watu hao walipopata upenyo na kutokomea.


Alisema alipelekwa katika hospitali ya Mkoa Mt Meru na kisha kuhamishiwa katika hospitali ya St Elizabeth na kulazwa na baadaye  kushonwa nyuzi zaidi ya 30 katika  jeraha la mkono .

Palangyo alisema tayari uongozi wa mgahawa huo umetoa taarifa polisi juu ya tukio hilo na polisi wameanza uchunguzi wa kuwakamata wahusika wa tukio hilo.

Akiongea kwa masikitiko meneja huyo, Helen Simba mkazi wa Ungalimited alisema kuwa siku ya tukio akiwa eneo Lake la kazi alivamiwa na vijana wawili akiwa amelala chumbani kwake katika mgahawa huo baada ya kuvunja mlango wa chumba chake.
Heleni Simba,meneja wa Mgahawa baaada kunusurika


Alisema kuwa vijana hao wawili walikuja kama wateja katika mgahawa huo wakitaka huduma ya chakula cha sh 5000 hata hivyo Helen aliwaambia kuwa hakuna chakula cha bei hiyo ndipo vijana hao waliendelea kukaa eneo hilo na yeye kuingia chumbani kupumzika.

Aidha alisema akiwa chumbani ghafla alishtukia kuona watu wawili wameingia  bila kujua na kuanza kumvua suruwali huku wakimpiga ngumi za uso na kichwani na baadaye mmoja wapo alivunja chupa na kumchoma kwenye mkono wake wa kushoto.

Aliongeza kuwa wakati tukio hilo likifanyika mtu mmoja wa tatu  alikuwa akimchukua video na baadaye walitokomea kusikojulikana baada ya watu kupiga kelele za tukio hilo.

Heleni ameliomba jeshi la polisi mkoani hapa kumsaidia kuwasaka watu hao ili wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Justine Masejo hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo
Jitihada za kumtafuta Inaendelea.
Ends...

Post a Comment

0 Comments