MAPATO YA UTALII YAHUJUMIWA ..WATALII WADAIWA KULIPIA KWENYE NCHI ZAO

 

Katibu mkuu TTGA,Robert Max 

Na Joseph Ngilisho, Arusha 


Wadau wa sekta ya utalii Mkoani Arusha wameiomba serikali kuchunguza baadhi ya makampuni ya kigeni ya utalii ambayo wageni wake hulazimika kulipia huduma za utalii kwenye nchi wanazotoka badala ya kulipia hapa nchini na hivyo kuikosesha mapato serikali ya Tanzania. 


Wakiongea kwenye kikao kazi cha utalii jijini ,Arusha, kilichoandaliwa na ubalozi wa uholanzi kwa kushirikiana na European Business  Group Tanzania (EUBG) kilicholenga kukuza sekta ya utalii na kuangalia namna bora ya uwekezaji.


Mwenyekiti wa chama cha waongoza utalii Tanzania(TTGA) Halfa Msangi alisema ipo haja kwa serikali kutazama upya  wamiliki wa kampuni za kigeni za utalii hapa nchini, ambapo inadaiwa kuwa wageni wao hulipia huduma hiyo kwenye nchi zao kabla ya kutua nchini na hivyo kuikosesha mapato serikali.


"Pande zote mbili zinahitaji kukaa chini ili kuona namna ya kunufaika na mapato ya utalii kwa sababu mali ipo Tanzania lakini wanaonufaika na kodi kubwa ni nchi zilizopo nje ya Tanzania "alisema Msangi 


Naye katibu mkuu wa TTGA,Robert Max alisema suala la uwekezaji linapaswa kuwa na manufaa kwa wazawa na taifa kwa ujumla kwa kuzitaka kampuni za kigeni kulipia huduma hapa nchini na siyo nje ya nchi ili kuifanya serikali ipate kodi ya moja kwa moja.


"Mfano mgeni analipia dola 10000 kwenye kampuni fulani inayomiliki hoteli hapa nchini sasa kwanini hiyo pesa isilipiwe hapa nchini ili serikali izidi kupata mapato yake ila kinacho fanyika hizo pesa zikilipiwa nje ya nchi huku nchini zinakuja pesa za kuendesha kampuni kama mishahara na mafuta ya magari". Alisema Max.


"Rai yetu kwa Serikali tunaomba pesa zote zinazo lipwq nje ya nchi kwaajili ya huduma hapa Tanzania tunaomba zilepwe hapa hapa Tanzania kwa kufanya hivyo serikali itapata kodi yake staking kulipo kulipiwa kwenye nchi za kigeni". Aliongeza Max.


Aidha alieleza kwamba  swala  la kulipia kodi nchi za kigeni na huduma kutolewa Tanzania ni jambo la ajabu ambalo halina maana na faida kwa maendeleo ya nchi na sekta ya utalii kwa ujumla maana fedha hizo zinazo potelea nje ya nchi zingeweza kufanya kazi ya kutengeza barabara za hifadhini na kuboresha huduma za afya hata elimu.


"Haiingii akilini Hotel ipo Tanzania na fedha inalipiwa nje ya nchi, tunaiomba serikali kupitia mamlaka ya mapato nchini TRA kuchukua hakua za haraka kuinusuru hii sekta kwa kuangalia namna hizi fedha zinazo lipwa nje ya nchi katika hotel zilizopo hapa nchini". Alisema Max.


 "Ili sekta ya utalii ikuwe zaidi na sekali kunufaiika inatakiwa viongozi wote waangali upya sera zetu na kuhakikisha zinarekebishwa ili kuweka usawa wa makampuni yote hapa nchini yanayo husika na swala zima la utalii maana jambo hili linatuumiza katika uwekezaji na ukuaji wa sekta yetu ya utalii".


Naye katibu wa chama cha wasafirishaji  watalii TATO,Cyril Ako alisema jitihada kubwa zinafanyika ili kurekebisha sera za utalii na tayari baadhi zimekuwa zikifanyiwa kazi na kupelekea kuongezeka kwa uwekezaji katika sekta ya utalii. 

Katibu mkuu TATO,Cyril Ako.
 




Alisema biashara ya utalii ni mnyororo wa thamani ambapo serikali inapaswa kuhakikisha inafuatilia mapato zaidi ya utalii hasa maeneo yanayodhaniwa, watalii kulipia huduma za utalii kwenye nchi zao.


Ends...

Post a Comment

0 Comments